marehemu omariomari enzi za uhai wake
Ndugu na jamaa wakiwa na
majonzi msibani kwa marehemu Omar Omar, Temeke-Mikoroshini jijini
Dar.
Mwanamuziki wa kizazi kipya, Dully Sykes, mwenye T-shirt ya
mistari (nyuma katikati) akibadilishana mawazo na wazee msibani
hapo.
Meneja wa marehemu, Bonga Ticha (kushoto) akiwa na meneja wa
kundi la muziki la Wanaume Family, Mkubwa Fella.
----------------------
WAOMBOLEZAJI mbalimbali
wakiwemo wasanii wa muziki wa kizazi kipya, leo wamekusanyika nyumbani kwa
mwanamuziki mkongwe wa miondoko ya mnanda, Omar Omar Mfungilo, aliyefariki dunia
usiku wa kuamkia leo nyumbani kwao Temeke-Mikoroshini, Dar es Salaam. Kwa mujibu
wa baba mdogo wa marehemu, mzee Yusufu Ally Mfungilo, marehemu Omar anatarajiwa
kuzikwa kesho saa saba mchana huko Temeke.
Post a Comment