Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MSTAAFU WA IKULU ALIA NA RAFU ALIYOFANYIWA NA SERIKALI ILIYOPO MADARAKANI

 Rubani Mstaafu wa Ndege za Serikali, Felix Henry Kileo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana juu ya tukio la kuvinjiwa nyumba namba 15 aliyokuwa akiishi na kufanya biashara katika kitalu namba 223/50 kilichopo mtaa wa Ohio jijini humo. Kwa Mujibu Wa wakala wa Majengo wa Serikali (TBA) Kiwanja hicho kinamilikiwa na Benki ya Uwekezaji Tanzania (TIB) na Benki hiyo inataraji kujenga Makao makuu ya Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB). 

Rubani huyu alidai kitendo cha kubomolewa nyumba yake ni cha kinyama kwani yeye alikuwa mtumishi wa serikali kama rubani na katika kipindi chote cha utumishi wake hakuwahi hata siku moja kupata ajali hata pancha akiendesha Viongozi kama Marais.

TINGATINGA likivunja nyumba iliyopo mtaa wa Ohayo kitalu namba 15 iliyokuwa inamilikiwa na Kapteni Msataafu wa Ndege ya Rais Felix Kileo Chini ya Kampuni ya udalali ya Rhino Auctionmart, kwa madai kuwa kampuni hiyo imepewa kazi hiyo ya kubomoa na tassisi ya Benki ya Wakulima TIB. Kwamujibu wa maelezo ya wabomoaji hao TIB  wanataka kujenga jengo la ghorofa kwenye eneo hilo, baada ya nyumba hiyo kupewa na serikali na mtumishi wa serikali aliyekuwa anaishi kwenye nyumba hiyo kupewa nyumba nyingine lakini alikaidi kutoka ndio maana kampuni hiyo imeingia kwa kuvamia nakuanza kuvunja.

Vitu vikiwa nje 
Vyombo vilivyokuwa vikitumika upande wa Biashara vikiwa nje.Mgahawa ulikuwa maarufu kama Kwa Mama.

Hizi ndio barua zenye maelezo kamili juu ya sababu ya kubomolewa nyumba hizo na lengo ni nini la Ubomoaji huo.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top