Kamanda
wa jeshi la polisi mkoa wa Singida (wa kwanza kushoto mwenye fimbo) akiangalia
daraja lililobomoka la Munung’una lililopo barabara kuu ya Singida – Mwanza eneo
la kijiji cha Msisi wilaya ya Singida.
Mhandisi
wa TANROADS mkoa wa Singida,Yustaki Kangole akiwaelekeza jambo wahandisi wa
kampuni ya CHICO iliyojenga daraja lililobomokajuzi la kijiji cha Msisi wilaya
ya Singida.Daraja hilo lililopo kwenye barabara kuu ya Singida –
Mwanza,limebomoka baada ya kuzidiwa na maji ya mvua kubwa iliyonyesha siku moja
kabla ya mwaka mpya.
Baadhi
wa wasafiri waliokwama baada ya daraja la Munung’una lililopo katika barabara
kuu ya Singida – Mwanza eneo la kijiji cha Msisi wilayani Singida, kubomoka juzi
kufuatia mvua kubwa zilizonyesha mkoani Singida.athaniel
Limu
Mvua
kubwa zinazoendelea kunyesha mkoani Singida,zimeendelea kuleta maadhara makubwa
ikiwemo kuvunja daraja na barabara kuu ya Singida – Mwanza na kuua raia moja wa
nchini China.
Juzi
mvua hizo zilisababisha familia ya watu wanne ya wilaya ya Mkalama mkoa wa
Singida, kupoteza maisha baada ya kuangukiwa na nyumba ya
tembe.
Mvua
hizo kubwa zilizonyesha kuanzia mwaka mpya (1/1/2013) saa nane mchana hadi saa
12.30 jioni zilisababisha daraja la Munung’una lililopo katika kijiji cha Msisi
wilayani Singida, barabara kuu itokayo Singida kuelekea mikoa ya Kanda ya Ziwa
na nchi jirani za Kongo, Burudi, Rwanda na Uganda, kubomoka na kusabaisha shimo
kubwa.
Kubomoka
kwa daraja hilo kumechangia foleni kubwa ya magari yanayokadiriwa kuwa ni zaidi
ya mia tatu. Pia mawasiliano kati ya mikoa mbalimbali ikiwemo ya Kanda ya Ziwa
na nchi jirani yamekatika.
Mmoja
wa madereva walioathirika na kubomoka kwa daraja hilo, George Medadi, aliyekuwa
akitokea Mwanza akirudi jijini Dar-es-salaam, alisema kubomoka kwa daraja hilo
limechangiwa kwa kiasi kikubwa na kujengwa chini ya
kiwango.
“Wenyeji
wa hapa wametueleza kuwa kalvati zilizotumika ni zile za zilizowekwa wakati
Nalaila Kiula alipokuwa Waziri wa Ujenzi. Kampuni ya CHICO iliyojenga barabara
hii kwa kiwango cha lami waliyatumia makalivati hayo hayo na walichofanya ni
kulundika udogo juu tu,” Medadi alisema.
Naye
dereva Iddi Mussa alisema kuwa barabara nyingi zinazojengwa na kampuni za
kichina zimekuwa hazisimamiwi ipasavyo kitendo kinachochangia kuharibika haraka
na kuisababishia serikali kuingia hasara kubwa.
Kwa
upande wake Mkuu wa Wilaya ya Singida, Mwalimu Queen Mlozi alisema kwa kuanzia
wameimarisha ulinzi katika eneo hilo pamoja na kufungua kituo kidogo cha kutolea
huduma ya afya na kudhibiti uwezekano wa kutokea kwa magonjwa ya
mlipuko.
“Pia
tumefungua barabara ya Singida-Ndago –Misigiri kwa ajili ya kutumiwa na mabasi
ya abiria na yale yenye uzito chini ya tani kumi. Vile vile tunaangalia
uwezekano wa kuangalia ni namna gani watu waliokwama wanapata chakula,”
alisema.
Meneja
wa TANROADS Mkoa wa Singida, Mhandisi Yustaki Kangole, ambaye alifika na
wahandisi wa kampuni ya CHICO, alisema kuwa wamekubaliana na CHICO kwamba
wafukie shimo hilo kwa vifusi vya mawe makubwa ili barabara hiyo ianze kutumika
mapema iwezekanavyo.
“Kwa
sasa tunafanya kazi hii ya muda na baada ya eneo hili kukauka ndio ukarabati
mkubwa utafanywa ili kuimarisha barabara hii muhimu kwa uchumi wa taifa,”
alisema Mhandisi Kangole.
Wakati
huo huo, Mkuu wa Wilaya ya Mkalama, Edward Ole Lenga amesema kuwa raia moja wa
China amefariki dunia baada ya gari lake kusombwa na maji ya mto jirani na
kijiji cha Gumanga.
Alisema
Mchina huyo ambaye jina lake bado halijatambuliwa hadi sasa, alisombwa na maji
ya mto juzi majira ya jioni wakati akikatisha mto wa kijiji cha Gumanga wilaya
ya Mkalama. Ndani ya gari hilo alikuwa na mtoto wake ambaye alinusurika
kufa.
Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Singida, Linus Sinzumwa, alikiri kutokea kwa tukio hilo na
kusema kuwa taarifa zaid atatoa baadae.
Post a Comment