Naibu Waziri Ofisi ya
Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Ndugu Agrey Mwanri
akitoa maelekezo mbalimbali kwa uongozi wa Mkoa wa Rukwa katika majumuisho ya
ziara yake iliyodumu kwa muda wa siku saba Mkoani Rukwa ambapo alitembelea
miradi zaidi ya 22 ambayo baadhi yake aliiwekea mawe ya msingi. Katika hotuba
yake hiyo alitoa maagizo mbalimbali ambayo yote yalikuwa yakilenga kwenye
utawala bora, matumizi bora ya fedha za Serikali katika miradi pamoja
utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010. Katika hotuba yake
iliyodumu kwa zaidi ya saa tatu alizionya halmashauri zote nchini zitakazopata
hati chafu kuwa hazitapata fedha ya ruzuku ya miradi ya maendeleo (LGCDG-Local
Government Capital Development Grant) ikiwa ni kutoa funzo kwa watendaji wa
halmashauri pamoja na kupandisha hasira za madiwani ili waweze kuisimamia vizuru
halmashauri husika.
Mama Grace Mwanri, mke wa
Naibu Waziri wa TAMISEMI Agrey Mwanri akitoa ushuhuda kuhusu utendaji wa mumewe
"Anavyoongea na kutenda mume wangu ndivyo alivyo hata nyumbani na si kwamba
anafanya hivyo kupata sifa wala umaarufu kwani mara zote huwa hapendi mambo ya
kipuuzipuuzi" alisema mama Mwanri.
.
.
Katibu Tawala Mkoa wa Rukwa
Alhaj Salum Mohammed Chima akizungumza kuwatambulisha wageni na washiriki katika
kikao hicho cha majumuisho kwa mgeni rasmi Ndugu Agrey Mwanri kushoto. Katika
hotuba yake fupi alimuhakikishia Naibu Waziri kuwa maagizo yote aliyoyatoa
kwenye ziara yake yatafanyiwa kazi na kwamba miradi iliyokuwa na mapungufu
itarekebishwa.
Naibu Waziri Mwanri akizungumza
na washiriki wa kikao hicho ambacho kilihudhuriwa na makundi mbalimbali wakiwemo
viongozi wa Dini, Chama na Serikali. Taasisi za Umma, mashirika binafsi,
wajasiriamali, na watumishi mbalimbali wa halmashauri na taasisi za
Umma.
Sehemu ya washiriki wa kikao
hicho katika ukumbi wa RDC katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Rukwa wakifuatilia
hotuba ya majumuisho ya Ndugu Mwanri.
Kutoka kushoto ni Katibu Tawala
Msaidizi Utawala na Rasilimali Watu Mkoa wa Rukwa Ndugu Samson Mashalla na Kaimu
Katibu Tawala Wilaya ya Sumbawanga Ndugu Festo Chonya wakifuatilia kikao
hicho.
Baadhi ya wadau walioshiriki
kikao hicho wakifuatilia kwa makini, wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa
Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga Ndugu Godfrey Shona, Kaimu Mkurugenzi
manispaa ya Sumbawanga, Mbunge Mst. na muwekezaji wa ndani Ndugu Chrissant
Majiyatanga Mzindakaya na kwa kwanza kulia ni muwekezaji wa ndani Ndugu Reina
Lukara.
Naibu Waziri wa TAMISEMI Agrey
Mwanri akimkabidhi maagizo yatokanayo na ziara yake ya siku saba Mkoani Rukwa
Katibu Tawala wa Mkoa huo Alhaj Salum Mohammed Chima aweze kuyafanyia kazi
katika Mkoa wake.
Naibu Waziri wa TAMISEMI Agrey
Mwanri akimkabidhi maagizo yatokanayo na ziara yake ya siku saba Mkoani Rukwa
Mkuu wa Wilaya ya Kalambo Ndugu Moshi Chang'a aweze kuyafanyia kazi katika
Wilaya yake.
Naibu Waziri wa TAMISEMI Agrey
Mwanri akimkabidhi maagizo yatokanayo na ziara yake ya siku saba Mkoani Rukwa
Mkuu wa Wilaya ya Nkasi Ndugu Idd Kimanta aweze kuyafanyia kazi katika Wilaya
yake.
Naibu Waziri wa TAMISEMI Agrey
Mwanri akimkabidhi maagizo yatokanayo na ziara yake ya siku saba Mkoani Rukwa
Mkuu wa Wilaya ya Sumbawanga Ndugu Mathew Sedoyeka aweze kuyafanyia kazi katika
Wilaya yake.Picha na Hamza Temba - Ofisi ya
Mkuu wa Mkoa Rukwa
Post a Comment