Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania , Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete(pichani), amefanya
uteuzi wa Wenyeviti wapya wa Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA) na Kampuni ya
Reli Tanzania (TRL).
Katika uteuzi huo Rais
Kikwete amemteua Prof. Joseph Msambichaka kuwa Mwenyekiti wa TPA na kutengua
uteuzi wa Bwana Raphael Mollel, ambaye alikua anashikilia wadhifa huo. Prof.
Msambichaka ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Mbeya.
Rais Vilevile amemteua
Bwana Severine M.A Kaombwe, kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya TRL. Bwana Kaombwe ni
Mtaalam wa Usafirishaji (East Africa Corridor Diagnostic Study for Northern and
Central Corridors).
Kulingana na Kaimu
Katibu Mkuu Kiongozi Bw. Peniel Lyimo, uteuzi huu unaanza tarehe 16 Januari,
2013.



Post a Comment