Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

SHEHENA YA PEMBE ZA NDOVU ZANASWA MTO WA MBU KIBAONI ARUSHA.

 

Picha ya maktaba ya membo ya tembo.

Picha ya tembo.

SHEHENA ya meno ya Tembo ambayo kiwango chake hakijajulikana, imekamatwa katika eneo la Mto wa Mbu Kibaoni, ikiwa katika gari aina ya Land Cruser GX lenye namba za bandia.

Gari hilo limekutwa likiwa na namba za bandia T 164 APZ, lakini lilipochunguzwa katika vioo vyake lilionekana lina namba za Serikali ambazo ni STK 3216.

Habar iza kuaminika ambazo MTANZANIA imezipata ni kwamba gari hilo linasemekana linatumiwa na mwambata wa jeshi katika nchi moja iliyo kusini mwa Afrika ambaye yupo nchini.



Taarifa za uhakika kutoka vyanzo vya jeshi la polisi na Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA), zinasema gari hilo lilikamatwa majira ya saa saba usiku wa kuamkia jana.

Taarifa hizo zinasema baada kukamatwa alikutwa dereva wa gari hilo ni Sajenti wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) aliyetambulika kwa jina la Aziz Athumani.

Taarifa hizo zinasema, mbali ya shehena hiyo pia ilikutwa bunduki aina ya Rifal.

Sajenti huyo anashikiliwa makao makuu ya polisi mkoani Arusha, akisaidia kutoa uchunguzi wa jambo hilo.

Habari kutoka vikosi vya usalama mkoani Arusha zinasema kwamba, kukamatwa kwa shehena hiyo kumetokana na kazi iliyofanywa na kikosi maalumu cha doria kinachopambana na na masuala ya ujangili.

“Kikosi hiki kinaendelea kufanya uchunguzi ili kubaini iwapo namba za gari hilo ni za Serikali au laa. Baada ya hapo taratibu nyingine za kisheria zitafuata,” kilisema chanzo hicho.

Kikosi hicho kinaundwa na askari wa Mamlaka ya Hifadhi ya Taifa (TANAPA), Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro pamoja na makachero wa Jeshi la Polisi.

Taarifa hiyo inasema gari hilo lilikurupushwa na maofisa hao wa kikosi maalumu, ambapo wakati likikimbia ndipo lilipopata ajali katika eneo hilo la Mto wa Mbu Kibaoni.

Hata hivyo inasadikiwa baadhi ya watu waliokuwa ndani ya gari hilo walifanikiwa kutoroka wakiwa na shehena nyingine ya meno ya Ndovu.

Katika harakati hizo, dereva wa gari hilo Sajenti Athumani ambaye alikuwa akiendesha gari hilo alishindwa kukimbia na hivyo kujikuta akiangukia katika mikono ya kikosi hicho maalumu.

Miongoni mwa watu wengine wanaotajwa kutoroka, ni pamoja na mkazi mmoja wa jijini Arusha aliyetajwa kwa jina moja la Frank, ambaye jina lake limekuwa likihusishwa na shughuli za ujangili mkoani humo.

Habari zaidi kutoka eneo la tukio zinasema kwamba, baada ya kukamatwa kwa gari hilo kulizuka mvutano mkubwa miongoni mwa maofisa hao wa TANAPA, Polisi wa Ngorongoro kuhusu kutangazwa kwa taarifa hizo.

Hii si mara ya kwanza kwa shehena za meno ya Tembo kukamatwa katika maeneo mbalimbali nchini, ambayo yamekuwa tishio kwa maisha ya wanyama hao.

Kumekuwapo na matukio mengi ya kukamatwa kwa meno ya Tembo, ambayo yamekuwa yakihusisha ujangili katika hifadhi za taifa.

Matukio haya yamekuwa yakitokea wakati Serikali ikitangaza kuwa inapambana na makali ya ujangili yanayotishia uhai wa wanyama kama tembo, faru na wengineo.

Hivi karibuni Polisi mkoani Ruvuma iliwakamata watu wanne wakazi wa Dar es Salaam, kwa tuhuma za kukutwa na vipande 80 vya meno ya Tembo, yenye uzito wa kilo 71.3 yenye thamani ya Sh milioni 6.4.

Kamanda wa Polisi mkoani humo Michael Kamuhanda, alisema askari wa doria waliwakamata watu wanne wakiwa wamebeba vipande vya meneo hayo ambayo yalikuwa yamepakiwa katika gari iliyokuwa imebandikwa namba za bandia DFP 7208 Toyota Land Cruiser.

Kamanda Kamuhanda alisema uchunguzi uliofanywa na Polisi ulibaini kuwa meno hayo yalikuwa yakisafirishwa kutoka Namtumbo kwenda Dar es Salaam.

Jeshi la Polisi mkoani Morogoro nalo mwishoni mwa mwaka jana liliwakamata vijana watatu, akiwemo mwenye umri wa miaka 17, eneo la Maseyu katika barabara kuu ya Morogoro-Dar es Salaam, wakisafirisha meno 51 ya Tembo kutoka Mbeya kuelekea Dar es Salaam.

Walikuwa wakitumia gari ya Toyota Land Cruiser walilokuwa wamelibandika namba bandia za DFP 3468 zikiwa na tofauti na namba halali za gari hiyo zilizokuwa zimeandikwa kwenye vioo T 949 ATZ.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Adolphin Chialo, aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni mtoto mwenye umri wa mika 17, Anael Mkinda, mkazi wa Shinyanga ambaye ni fundi magari.

Wengine ni Amir Adrian (26) na Eric Kihamzi (25) wote ni madereva. Vijana hao walidaiwa walikuwa doria katika barabara hiyo walilishitukia gari hilo baada ya kuona namba zake za usajili hazina ubora, tofauti na thamani ya gari hilo.

Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top