WAKATI wananchi wengi wakiguswa na msiba wa msanii wa filamu Tanzania, Sadick Juma Kilowoko ‘Sajuki’, wengine wameanza kuutumia msiba huo kwa kufanya utapeli.
Jamaa mmoja mkazi wa Sinza jijini Dar es Salaam, anayefahamika kwa jina la Tumainielly Kitula, anafanya utapeli wa kuwarubuni wananchi kuwa ametumwa na familia ya marehemu kukusanya michango kwa ajili ya msiba. Mwenyekiti wa Kamati ya Fedha ya Mazishi ya Sajuki, Michael Sangu ‘Mike’ amesema jamaa huyo amejikusanyia fedha na ameweka namba yake kwenye Mtandao wa Facebook.
Mtuhumiwa alipigiwa kupitia namba 0656111551 na kujifanya kama ni shabiki wa Sajuki, ndipo tapeli huyo alisema yeye ni ndugu wa marehemu na anapokea michango.
Mike alisema: “Wananchi wawe na makini na matapeli, mtu pekee aliyekabidhiwa jukumu la kupokea fedha ni mimi.”
Maziko yatafanyika leo saa saba na nusu mchana katika makaburi ya Kisutu.
Post a Comment