Kamati ya Uchaguzi ya
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imeahirisha uchaguzi wa Chama cha
Makocha wa Mpira wa Miguu Tanzania (TAFCA) uliokuwa ufanyike leo (Januari 19
mwaka huu) jijini Dar es Salaam.
Uchaguzi umeahirishwa
kwa vile ulitaka kufanyika bila kuzingatia Katiba ya TAFCA Ibara ya 32(1) na
Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF Ibara ya 10(6) na 26(2), hivyo Kamati ya
Uchaguzi ya TFF imeahirisha uchaguzi huo kwa vile nafasi zilizoombwa kugombewa
na idadi ya waombaji uongozi haikidhi matakwa ya Katiba ya
TAFCA.
Pia taratibu za kikanuni
ikiwa ni pamoja na kuwaarifu waombaji uongozi ambao hawakukidhi matakwa ya
Katiba ya TAFCA hazikukamilika kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa
TFF.
Licha ya upungufu huo,
TAFCA haikuwasilisha taarifa za mchakato mzima kama ilivyoombwa na TFF. Kamati
ya Uchaguzi ya TFF imeiagiza Kamati ya Uchaguzi ya TAFCA kuandaa uchaguzi mpya
utakaokidhi matakwa ya Kamati ya TAFCA baada ya Uchaguzi Mkuu wa
TFF.
TFF inaishauri TAFCA
kutumia fursa ya Mkutano Mkuu wa leo (Januari 19 mwaka huu) kujadili mustakabali
wa TAFCA kwa kuwa chama hicho kimeshindwa mara mbili kupata idadi ya wagombea
wanaokidhi akidi ya Kamati ya Utendaji.
Pia TAFCA haijawahi
kufanya mikutano ya Kamati ya Utendaji na Mkutano Mkuu kwa karibu miaka
minne.
Boniface
Wambura
Ofisa
Habari
Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF)


Post a Comment