 |
| Waziri
wa Maji na Umwagiliaji wa Serikali ya Misri Prof. Dr. Mohamed Bahaa
El-Din Ahmed akionja ladha ya maji toka kwenye bomba kuu la chanzo cha
maji yanayoelekezwa kwenye bomba la utekaji maji kijiji cha Mwanang'ombe
wilayani Maswa mkoani Simiyu ikiwa ni moja kati ya hatua za serikali ya
Tanzania kusaidia wananchi wake kukabiliana na tatizo la upatikanaji wa
maji salama. |
 |
| Waziri
wa Maji na Umwagiliaji wa Serikali ya Tanzania Jumanne Maghembe naye
akionja ladha ya maji toka kwenye bomba kuu la chanzo cha maji
yanayoelekezwa kwenye bomba la utekaji maji kijiji cha Mwanang'ombe
wilayani Maswa mkoani Simiyu ikiwa ni moja kati ya hatua za serikali ya
Tanzania kusaidia wananchi wake kukabiliana na tatizo la upatikanaji wa
maji salama. |
 |
| Mbunge
wa jimbo la Busega mkoani Simiyu Titus Kamani naye akionja ladha ya
maji toka kwenye bomba kuu la chanzo cha maji yanayoelekezwa kwenye
bomba la utekaji maji kijiji cha Mwanang'ombe wilayani Maswa mkoani
Simiyu ikiwa ni moja kati ya hatua za serikali ya Tanzania kusaidia
wananchi wake kukabiliana na tatizo la upatikanaji wa maji salama. |
 |
| Mama
Maria akiondoka kwenye eneo la bomba kuu la kutekea maji mara baada ya
kutwishwa ndoo na Waziri wa Maji na Umwagiliaji wa Serikali ya Misri
Prof. Dr. Mohamed Bahaa El-Din Ahmed huku wananchi wengine wakipiga
makofi kuashiria kufurahia tukio hilo lililofanyika katika kijiji cha
Mwanang'ombe wilayani Maswa mkoani Simiyu. . |
 |
| Jiwe la Msingi. |
 |
| Ni burudani ya ngoma ya kabila la wasukuma na wala si mchezo wa vita. |
 |
| Meza
kuu ikifurahia yanayojiri ya kiburudani katika kijiji cha Mwanang'ombe
wilayani Maswa mkoani Simiyu kwenye ufunguzi wa visima 30 katika maeneo
ya wilaya sita kame, Tanzania vilivyochimbwa kwa msaada wa serikali ya
Misri . |
Kwa
upande wake waziri wa Maji na Umwagiliaji Nchini Prof. Jumanne Magembe
amesema kuwa Serikali imejipanga vyema kuhakikisha inapunguza kama si
kuondoa kabisa tatizo la uhaba wa maji nchini Tanzania.
Bofya Play usikilize ..
Takwimu
za upatikanaji wa maji katika Wilaya zilizochaguliwa kwenye mradi huo
hadi mwezi Disemba 2011 katika wilaya zilizomo kwenye miradi zinaonyesha
kuwa na hali ni ya mvua zisizoridhisha, hivyo kipaumbele katika mradi
huu ni kusaidia kwanza maeneo yaliyo upande wa mvua kidogo ambapo
matarajio ya serikali kwa miradi yote ikikamilika hali ya upatikanaji wa
maji katika vijiji vyote itakuwa bora, suala ambalo linawezekana.
Nae
Waziri wa Maji na Umwagiliaji wa Serikali ya Misri Prof. Dr. Mohamed
Bahaa El-Din Ahmed amesema kuwa serikali yake inajivunia msaada
iliyoutoa wa kiasi cha fedha Dola milioni moja za Kimarekani kusaidia
kukamilika kwa miradi ya maji nchini Tanzania kwani Misri inaamini kuwa
hiyo ni moja kati ya njia ya kudumisha na kuendeleza ushirikiano
uliopo.
Msaada
huo wa Misri si suala geni hapa nchini kwani tangu enzi za hayati Baba
wa Taifa Mwl. Nyerere, Tanzania na Misri zimekuwa zikishirikiana katika
Nyanja za siasa, maji, kilimo cha umwagiliaji, na Tanzania imekuwa
ikipokea madaktari wakujitolea ambao wamekuwa wakifanya kazi kwenye
hospitali za mikoa na kila mwaka Tanzania imekuwa ikipeleka wataalamu
wake nchini Misri kupata mafunzo kujinoa katika taaluma hiyo.
 |
| Wananchi
wa kijiji cha Mwanang'ombe wilayani Maswa mkoani Simiyu wakisikiliza
hotuba za viongozi kwenye ufunguzi wa visima 30 katika maeneo ya wilaya
sita kame, Tanzania vilivyochimbwa kwa msaada wa serikali ya Misri |
Pamoja
na mradi huu, huduma ya maji imeendelea kuboreshwa kote nchini kupitia
Program ya maendeleo ya Sekta ya Maji ambayo ilianza kutekelezwa tangu
mwaka 2006, kwa kushirikisha juhudi za wananchi wenyewe na washirika
wengine wa maendeleo. Miradi inayoendelea kutekelezwa kwa fedha za
programu wilayani Maswa ni ; Miradi ya maji ya bomba ya vijiji vya
Sayusayu, malampaka na Mwasayi; Miradi mipya inayokaribia kuanza
kutekelezwa ni ya vijiji vya Njiapanda na Jija.
Lengo la Programu ya Maji ni kuwa kufikia mwaka 2015,huduma ya maji vijijini iwe wastani wa asilimia 65.
 |
| Wananchi
wa kijiji cha Mwanang'ombe wilayani Maswa mkoani Simiyu wakisikiliza
hotuba za viongozi kwenye ufunguzi wa visima 30 katika maeneo ya wilaya
sita kame, Tanzania vilivyochimbwa kwa msaada wa serikali ya Misri |
Wito
umetolewa kwa wananchi wa kijiji hicho na maeneo yote ya miradi nchini
kuwa walinzi wa miundombinu ya maji. kutokomeza tatizo la miundombinu ya
maji na vifaa vya maji kuhujumiwa na watu wabaya ambao huing'oa na
kuuza kama chuma chakavu hivyo kila mwananchi awe mlinzi wa miundombinu
hiyo kwa faida ya taifa na kwa kuzingatia maslahi ya walio wengi
(kuwaepusha mama zetu na adha ya kusafiri umbali mrefu kusaka maji
salama).
Post a Comment