Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

Wabunge Uingereza waipongeza Tanzania

WABUNGE kutoka Bunge la Uingereza (House of Commons) wameisifu Tanzania kutokana na jitihada zake za kupambana na ugonjwa wa malaria na kusema ni mfano wa kuigwa barani Afrika.
Wakizungumza na waandishi wa habari juzi mjini Moshi, Wabunge hao walisema ili kudhibiti kuenea kwa ugonjwa wa malaria, uwekezaji mkubwa unahitajika katika nchi za Afrika ikiwamo Tanzania.
Wabunge hao walioko Kamati ya Bunge ya Malaria na Kilimo ni Jeremy Lefroy wa Jimbo la Stafford, Richard Bacon wa Jimbo la Norfolk Kusini na John Mann wa Jimbo la Nottinghamshire.
“Wasiwasi wetu sasa unatokana na hisia za watu kwamba ugonjwa wa malaria umetoweka wakaanza kutokuwa waangalifu na Tanzania ikatumbukia kwenye janga kubwa zaidi la Malaria”alisema Lefroy.
Mbunge huyo aliitaka Serikali ya Tanzania kuendelea kuwaelimisha wananchi wake kuhusu athari za ugonjwa huo na wasibweteke na mafanikio iliyoyapata katika mapambano dhidi ya ugonjwa huo.
Lefroy alisema walipotembelea kiwanda cha A to Z cha jijini Arusha kinachotengeneza vyandarua vye dawa za kudhibiti mbu waenezao malaria, walifurahishwa sana na juhudi za kudhibiti ugonjwa huo.
“Kutokana na juhudi hizo za Tanzania ambazo zimefanikishwa na ufadhili wa The Global Fund (mfuko wa dunia), Tanzania inaweza kuongoza mapambano ya malaria barani Afrika” alisema Lefroy.
Kwa upande wake, Mann alisema nchi yake ingependa kuona misaada ya kifedha ya kupambana na malaria inatumika kwa kazi hiyo na kuisifu Tanzania kuwa imekuwa kielelezo cha umakini katika hilo. Mbunge wa Norkfolik Kusini, Bacon alisema ugonjwa wa malaria unaathiri sana uchumi wa nchi husika na akayapongeza mashirika yasiyo ya kiserikali na taasisi za dini katika kupambana na malaria.
Nchi ya Uingereza ndiyo mchangiaji mkubwa wa mfuko wa dunia wa Global Fund na imekuwa ikichangia Pauni 190 milioni kila mwaka ambazo ni Sh380 bilioni za Tanzania kila mwaka.
Katikati ya mwaka jana, mfuko huo mahsusi kwa ajili ya kupambana na magonjwa makuu matatu ya Malaria, Kifua Kikuu na Ukimwi, uliidhinisha Dola 22.9 milioni kusaidia miradi 1,000za Marekani katika nchi 151.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top