WAMILIKI wa vyombo vya
habari nchini, (MOAT),wameaswa kuzingatia muda na wakati wa kurusha matangazo
katika vyombo vyao, kwa sababu baadhi yake yameonekana kupoteza maadili kwa
jamii hususani watoto ambao ni Taifa la baadaye.
Akizungumza
jijini Dar es Salaam jana, Katibu wa Taasisi ya kupambana na Udanganyifu wa
matumizi ya rasilimali za Taifa (CFRI), Andendekisye Mwakabalula, alieleza kuwa
kutokana na mfumo mbaya wa matangazo hususankatika televisheni
utasababisha madhara kwa kizazi hiki na cha baadaye.
Katika hilo, aliwataka
wamiliki hao kuangalia njia mbadala ambayo haitaleta madhara kwa jamii pindi wa
matangazo hayo yatakaporushwa au kuonyeshwa kwenye vyombo
hivyo.
Mwakabalula aliyataja
baadhi ya matangazo ambayo yanachochea uvunjifu wa maadili ni mfano wa matangazo
ya mpira wa kiume ‘kondomu’,filamu za ngono pamoja na mengine ambayo
hayafundishi maadili bali yanapotosha.
“Ikiwa wamiliki wa vyombo
vya habari wamebaini wazi kuwa maadili ya nchi yameporomoka, walitakiwa kuwa
mifano mizuri ya kuigwa ndani ya jamii, hususani kwa kutumia fursa ya matangazo
yanayoibadili katika suala zima la maadili” alisema
Mwakabalula
Aidha, alisema ikiwa
wamiliki hao watatumia vyombo vyao kuhamasisha juu ya maambukizi ya virusi vya
ukimwi (HIV), kupitia matangazo mbalimbali basi waangalia muda na wakati wa
kuyaonyesha kwa lengo la kutowaumiza watoto ambao hawajafikia umri wa
kuyasikiliza au kuyatizama.
Pamoja na hilo, aliitaka
Katiba mpya kupitia mchakato wa mapendekezo ya maoni ya wananchi, kuangalia
namna ya kuiweka kipengele cha mkakati huo wa matumizi ya matangazo ili kuleta
uwiano na manufaa ndani ya jamii.
Post a Comment