Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

WAMILIKI WA VYOMBO VYA HABARI NCHINI, (MOAT)WAASWA KUZINGATIA MAADILI

 

WAMILIKI wa vyombo vya habari nchini, (MOAT),wameaswa kuzingatia muda na wakati wa kurusha matangazo katika vyombo vyao, kwa sababu baadhi yake yameonekana kupoteza maadili kwa jamii hususani watoto ambao ni Taifa la baadaye.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Katibu wa Taasisi ya kupambana na Udanganyifu wa matumizi ya rasilimali za Taifa (CFRI), Andendekisye Mwakabalula, alieleza kuwa kutokana na mfumo mbaya wa matangazo hususankatika televisheni utasababisha madhara kwa kizazi hiki na cha baadaye.
Katika hilo, aliwataka wamiliki hao kuangalia njia mbadala ambayo haitaleta madhara kwa jamii pindi wa matangazo hayo yatakaporushwa au kuonyeshwa kwenye vyombo hivyo.
Mwakabalula aliyataja baadhi ya matangazo ambayo yanachochea uvunjifu wa maadili ni mfano wa matangazo ya mpira wa kiume ‘kondomu’,filamu za ngono pamoja na mengine ambayo hayafundishi maadili bali yanapotosha.
“Ikiwa wamiliki wa vyombo vya habari wamebaini wazi kuwa maadili ya nchi yameporomoka, walitakiwa kuwa mifano mizuri ya kuigwa ndani ya jamii, hususani kwa kutumia fursa ya matangazo yanayoibadili katika suala zima la maadili” alisema Mwakabalula
Aidha, alisema ikiwa wamiliki hao watatumia vyombo vyao kuhamasisha juu ya maambukizi ya virusi vya ukimwi (HIV), kupitia matangazo mbalimbali basi waangalia muda na wakati wa kuyaonyesha kwa lengo la kutowaumiza watoto ambao hawajafikia umri wa kuyasikiliza au kuyatizama.
Pamoja na hilo, aliitaka Katiba mpya kupitia mchakato wa mapendekezo ya maoni ya wananchi, kuangalia namna ya kuiweka kipengele cha mkakati huo wa matumizi ya matangazo ili kuleta uwiano na manufaa ndani ya jamii.
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top