· Wateja
kupata salio mara mbili kila anapotuma
pesa kupitia Airtel Money
- Ni kwa wateja wa malipo ya awali nchi nzima
Kampuni
ya simu za mkononi
ya Airtel leo imezindua
promosheni mpaya ya Airtel Money ambapo wateja wakel watapata muda wa maongezi
mara mbili ya gharama watakazotozwa kwa kutuma pesa na kupata wateja muda wa
maongezi kulingana na ada ya makato pale wanapotoa pesa kwa kupita huduma ya
Airtel money.
Akizungumza kuhusu
promosheni hiyo, Meneja Uhusiano Jackson Mmbando alisema” Tumewawezesha wateja
wetu kutumia huduma ya Airtel money na kufanya miamala mbalimbali ya pesa huku
tukisogeza huduma za kifedha karibu na makazi na sehemu zao za kazi , leo
tunayofuraha kuwazawadia wateja wetu waliojisajili nchini nzima muda wa
maongezi mara mbili ya gharama watakazotozwa kutuma pesa kupitia Airtel money na
pia tunawapa muda wa maongezi kulingana na ada watakayotozwa kutoa pesa pale
watakapo toa pesa kupitia Airtel money. Bonus hii ya muda wa maongezi itatumika
kupiga simu Airtel kwenda Airtel siku nzima , kwa siku nzima hadi saa sita
usiku.”
“Tunaendelea kuboresha
huduma yetu ya Airtel money na kuendelea kutoa suluhisho la huduma za kifedha
hasa katika maeneo yenye changamoto ya huduma za kibenki. kwa kupitia mtandao
wetu mpana ulioenea zaidi tuna wawezesha watanzania nchni nzima hasa wa maeneo
ya vijijini kupata huduma za fedha zilizo salama , nafuu na gharama nafuu
kupitia Airtel Money.
Promosheni hii ya pata muda
wa maongezi itaondoa Kampeni ya bure, na kuanzia sasa wateja wa Airtel
watazawadia muda wa maongezi kila wanapotuma na kupokea pesa kupitia huduma ya
Airtel Money”. Aliongeza Mmbando
Airtel bado inaendelea
kutoa huduma za mawasiliano za simu zenye ubora na gharama nafuu , kwa sasa
wateja wa Airtel wa malipo ya Awali wanatuma ujumbe mfupi was ms kwa shilingi
moja mara baada ya kutuma ujumbe mfupi wa kwanza kwa shilingi 125na kupiga simu
kwa senti 10 mara baada ya dakika mbili za
mwanzo
Post a Comment