Jengo la Coco Plaza ambalo kuna Ofisi za
CRDB.
Kaimu Meneja wa
benki ya CRDB tawi la Oysterbay, Godlisten Mtei
Kaimu Meneja wa benki ya CRDB tawi la Oysterbay,
Godlisten Mtei (kushoto) akitoa maelekezo ya huduma mbalimbali wanazotoa katika
tawi hilo jipya kwa Waziri wa zamani wa Elimu, Joseph Mungai. Tawi hilo
limefunguliwa hivi karibuni katika jengo la Coco Plaza jijini Dar es Salaam.
Katikati ni Ofisa Masoko wa benki hiyo, Nasib Kalamba.
Ofisa Masoko wa benki ya CRD, Nasib Kalamba
(katikati) akitoa ufafanuzi kwa mteja wa benki hiyo, waziri wa zamani wa Elimu,
Joseph Mungai kaatika tawi jipya la benki hiyo lililopo katika jengo la Coco
Plaza jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Meneja wa Tawi hilo, Godlisten
Mtei.
Ofisa wa benki ya CRDB, JacqlineSawe akitoa
maelekezo kwa mteja wa benki hiyo katika tawi la Oysterbay lililopo katika jengo
la Coco Plaza jijini Dar es Salaam.
Ofisa Masoko wa benki ya CRD, Nasib Kalamba (kushoto)
akitoa ufafanuzi kwa mteja wa benki hiyo, waziri wa zamani wa Elimu, Joseph
Mungai katika tawi jipya la Oysterbay jijini Dar es Salaam.
Wateja wakipata huduma.
Maofisa wa benki ya
CRDB wakiandisha wateha wapya katika eneo la Namanga jijini Dar es Salaam.
Kaimu Meneja wa
benki ya CRDB tawi la Oysterbay, Godlisten Mtei (kushoto) akitoa
maelekezo
ya huduma
mbalimbali wanazotoa katika tawi hilo jipya kwa Waziri wa zamani wa Elimu,
Joseph Mungai.
Ofisa wa benki ya CRDB, George Abraham kisaini
baadhi ya nyaraka za kibenki.
DAR ES SALAAM, Tanzania
BENKI ya CRDB, imefungua tawi jipya Osysterbay
jijini Dar es Salaam ikiwa na lengo la kuwafikia wateja wake, ambapo takribani
wateja 400 wamekuwa wakihudumiwa kila siku katika tawi hilo.
Tawi hilo limeanza kufanya kazi hivi karibuni,
ambapo limeonekana kuwa ni msaada mkubwa kwa wakazi wa Osysterbay na maeneo ya
jirani.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar
es Salaam, jana Kaim Meneja wa CRDB, Godlisten Mtei alisema lengo kubwa la
kupeleka tawi hilo ni kuwapa huduma kwa ukaribu wateja wao waliopo katika eneo
hilo.
Alifafanua kwamba, tangu kuanzishwa kwake tawi
limekuwa ni mkombozi kwa wateja mbalimbali wakiwemo wafanyabiashara wakubwa na
wadogo pamoja na watu mbalimbali.
“Tawi letu linatoa huduma zote za kibenki, na
tunazidi kuwakaribisha wateja wetu ili wajionee huduma bora zitolewazo na benko
yetu na pia tunatoa huduma mbalimbali zikiwemo za; Mashine ya kutoa na kuweka
fedha (ATM) ambayo hufanyakazi masaa 24”alisema.
Mtei alitaja huduma zingine kuwa ni pamoja na
TemboCardVisa, Akaunti ya Hundi na ya watoto inayojulikana kama Junior Account
pamoja, Malikia akaunti ambayo ni maalum kwa wanawake na Akaunti ya
Akiba.
Hata hivyo aliongeza kuwa, tawi hilo litakuwa
likitoa Akaunti ya Tanzanite, huduma za mikopo mbalimbali na huduma za bima ili
kuzidi kuwapatia huduma bora wateja wao.
Alisema kuwa tangu kuanzishwa kwake tawi
limekuwa likitoa huduma ya kibenki kwa kutumia Simu ya mkononi (SimBanking),
pamoja na Akaunti ya Wanafunzi ambayo inafahamika kama Scholar Account.
Meneja huyo aliwataka Wananchi na wateja wapya
kutumia tawi hilo pekee katika eneo hilo ili kupata huduma za kibenki badala ya
kutembea umbali mrefu kufuata huduma hizo kwenye matawi yaliyombali.
Katika hatua nyingine Meneja Mauzo wa benki hiyo
Richard Joseph alisema, katika harakati za kufanikisha wananchi wanajiunga na
benki hiyo wameamua kuweka tawi katika eneo la Namanga jijini Dar es Salaam
ambapo kwa siku zaidi ya watu 70 wanaojiunga na benki hiyo.
Post a Comment