Mkuu wa Wilaya ya Ilala Bw, Raymond Mushi,akielezea mafanikio ya Serikali ya awamu ya nne kwa kipindi hicho katika wilaya hiyo.
Mushi
amesema kuwa, Kiwango cha uzoaji taka ngumu kimefikia tani 550
kwa siku sawa na tani 198,000 kwa Mwaka ambapo amesema kiwango hicho ni asilimia
50% ya tani 1100 za taka zinazo zalishwa kwa siku.
“Kwa
sasa kiwango cha Uzoaji taka ngumu kinaridhisha kutokana na wilaya kupata
vitendea kazi vyenye uwezo Mzuri”, amesema Mkuu wa
Wilaya.
Amesema
kuwa Mafanikio hayo, ni Miongoni mwa Mafanikio Mengi ambayo Serikali hiyo
imeyafikia kwa kipindi chake tangu imeingia Madarakani na kusema kuwa wana
matumaini kuwa mpaka kufikia mwaka 2015, Manispaa hiyo itakuwa imefanikisha
Mengi.
Ameendelea
kusema kuwa, kufanikiwa kwa asilimia hizo kunachangiwa na kununuliwa kwa
Magari sita ya kukandamiza taka yenye Uwezo Mkubwa wa kubeba kati ya tani kumi
hadi 24 kwa Safari moja ikiwa ni pamoja na Kununuliwa kwa makasha ya taka 30 na
kuwekwa kwenye maeneo yenye uzalishaji Mkubwa wa
taka.
Ameendelea
kuyataja Mafanikio mengine yaliyopo katika Manispaa hiyo kwa kipindi cha mwaka
2005-2012 kuwa ni, Usambazaji maji ambapo amesema katika Mamlaka ya maji DAWASA
imeongeza visima virefu vya Maji kutoka visima 110 mwaka 2005 kufikia 195 na
visima vifupi 60 kwa mwaka 2012.
Amesema
kuwa, mafanikio hayo yameambatana na Uboreshwaji wa Huduma za Afya, Ardhi,
Kilimo Ujenzi pamoja na Elimu, ambapo Katika Afya Manispaa imefanikiwa kuongeza
idadi ya Vituo vya kutolea huduma kutoka 15 hadi 22 pamoja na Zahanati 20
kutoka 13 zilizokuwepo kwa mwaka
2005-2012
Post a Comment