Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

FREEMASONS NA HARAKATI ZA KIDINI DUNIANI


KUTOKANA na familia ya Freeman Illuminati bloodline kuanzisha chama cha ‘Priory de Sion’kilichokuwa na lengo la kuingiza mafundisho machafu ndani ya imani ya kweli, dunia ililazimika kusubiri awamu nne za utawala wa serikali moja kabla ya kuunganisha dini na serikali na kuwa kitu kimoja. Kumbuka kwamba Mungu hutumia namba 1 hadi 12 ambapo namba 4 humaanisha ‘ukomavu na kuvunwa kwa mazao’ – rejea Marko 4: 26 kwa mbegu njema na Yakobo 1:14,15.

Rais Nimrodi wa serikali ya awamu ya kwanza ndiye aliyepanda mbegu ya ‘tamaa’ ya kuanzisha serikali na dini moja itakayoitawala dunia nzima. ‘Tamaa’ ya rais Nimrodi ilitengeneza ‘mimba’ na kupelekea awamu ya pili ya serikali moja ya dunia chini ya Waamedi na Waajemi wakati huo Dario akiwa ndiye rais na ikulu ya serikali hiyo ikiwa katika eneo la Iran ya leo. Baada ya miongo kadhaa kupita, ‘Mimba’ hiyo ilileta mtoto aliyepewa jina la ‘dhambi’ wakati wa awamu ya tatu ya serikali moja ya dunia iliyoitwa Uyunani chini ya rais Alexander mkuu aliyeweka ikulu yake huko Ugiriki. Historia inatuambia kwamba rais Alexander mkuu alikuwa katili na aliyefanikiwa kuua mamia kama sio maelfu ya watu duniani kote.

Hatimaye mbegu ya ‘tamaa’ iliyopandwa na rais Nimrodi wa serikali ya awamu ya kwanza ilipotengeneza ‘mimba’ na kuzaa mtoto ‘dhambi’, mtoto huyo alikomaa baada ya kufikisha umri wa utu uzima. Sasa hakuitwa ‘mtoto’ tena bali jina lake lilibadilika na kuitwa ‘mauti’. Kumbuka kwamba kuna hatua nne za kukua na kukomaa kwa mbegu hadi wakati wa kuvunwa. Hivyo ndivyo ilivyokuwa wakati dunia yetu iliposhuhudia awamu nne za serikali moja ya dunia ambapo katika awamu ya nne palitokea mavuno yaliyoleta mazao ya muungano wa serikali na dini.

Ulikuwa ni utawala wa serikali ya awamu ya nne (Roman empire) chini ya rais Constantine aliyeweka ikulu yake huko Roma ndipo imani ya kweli ilipokufa baada ya rais huyo kuanzisha dini iliyochanganya ukweli na uongo kwa kutumia kanuni ya ‘Thesis x Antithesis = Synthesis.  Imani ya kweli ilikuwa ni ‘Thesis’ wakati imani ya kipagani iliyoanzishwa na Nimrodi ilikuwa ni ‘Antithesis’. Imani hizi mbili zilichanganywa na rais Constantine na kuzaa kitu kinachoitwa ‘Synthesis’ yaani mchanganyiko wa ukweli na uongo. Hiyo ilikuwa ni baada ya miaka mingi kupita tangu rais Nimrodi alipotamani kuanzisha mfumo wa utawala uliunganisha serikali na dini na kuwa kitu kimoja. Hiyo ilikuwa ni awamu ya nne ya utawala wa serikali moja ya dunia. Naam! Dini iliyoanzishwa huko Roma wakati wa awamu ya nne ya utawala wa serikali moja ya dunia chini ya rais Constantine ilikuwa ni matokeo ya mbegu ya ‘tamaa’ ya rais Nimrodi ya kuanzisha mfumo wa serikali iliyoungana na dini katika utawala wa dunia nzima.

Jambo hilo la kuunganisha serikali na dini pamoja na kuchanganya ukweli na uongo lilipigwa vita vikali na ‘waprotestant’ ambao hawakuwa tayari kuona ukweli wa neno la Mungu ukichanganywa na uongo. Hata hivyo ‘waprotestant’ hao hawakufanikiwa kutenganisha serikali na dini na ndipo wakamua kujitenga na dini iliyokuwa imeungana na serikali ili wapate kumuabudu Mungu katika roho na kweli.

Ilipofika mwaka 1798 kulitokea badiliko katika serikali iliyoungana na dini baada ya rais na kiongozi wa dini kukamatwa na kuuawa huko ufaransa. Baada ya kifo cha rais na kiongozi wa dini wa serikali moja ya dunia, ilionekana kana kwamba ndio mwisho wa mfumo wa utawala uliounganisha serikali na dini. Lakini haukuwa mwisho kwa sababu liliundwa taifa moja katika mji wa Roma likiwa linaendeleza mfumo wa kuunganisha serikali na dini. Taifa hilo likapewa jina la Vatican. Ndioo! Vatican ni nchi inayotawalaiwa na Papa akiwa ndiye rais na kiongozi wa dini pia. Sasa jina la serikali hiyo likaitwa ‘Roman Catholic’ yaani ‘ulimwengu wa Kirumi’. Maana ya neno ‘catholic’ ni ‘universal’ au iliyoenea dunia nzima. Serikali hii imeenea dunia nzima kutokana na uwepo wa wawakilishi (mabalozi) wa taifa hilo duniani kote. Ukilinganisha na mataifa mengine katika eneo la mraba, inawezekana taifa hili ndilo dogo kuliko mataifa mengine duniani kote lakini ni taifa lenye nguvu kubwa kuliko mataifa yote – usishangae!

Zimekuwepo juhudi za kuhakikisha kwamba dunia nzima inarudi kwenye mfumo wa utawala wa serikali na dini. Freemasons wamekuwa kwenye mipango ya muda mrefu latika kuhakikisha kwamba serikali moja ya dunia itakayounganisha dini na uchumi kwa pamoja inaundwa haraka iwezekanavyo. Serikali hiyo itakuwa imejengwa kwenye msingi uliowekwa na rais wa kwanza katika awamu ya kwanza ya utawala wa serikali moja ya dunia. Itakumbukwa kwamba rais Nimrodi alianzisha dini iliyoabudu miungu (sayari) 36 ambapo jumla ya miungu hao ilileta namba 666.

..... Safari ijayo tutaitazama namba 666 na uhusiano wake na Freemasons .... Endelea kuwa na NDGSHILATU BLOG mahala popote na wakati wowote .....
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top