Mke wa Rais na Mwenyekiti wa
Taasisi ya Wanawake na Maendeleo Mama Salma Kikwete akipokea zawadi za kimila za
kabila la Wafipa, wakati alipokutana na akina mama wa manispaa ya Sumbawanga
kwenye ukumbi wa Manispaa hiyo tarehe 25.2.2013.
PICHA NA JOHN LUKUWI WA
MAELEZO
Akiwa amevalia vazi la asili
la akina mama wa kabila la Wafipa, Mke wa Rais Mama Salma Kikwete anashiriki
kucheza ngoma ya kabila hilo kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Manispaa ya
Sumbawanga tarehe 15.2.2013.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya
Chama Cha Mapinduzi ambaye pia ni Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizindua rasmi
shina la wakereketwa la kikundi cha akinamama cha Upendo kilichoko katika makao
makuu ya wilaya ya Kalambo katika mji wa Matai tarehe 26.2.2013. Akinamama hao
wapatao kumi hujishughulisha na kazi ya kukamua mafuta ya
alizeti.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa
WAMA Mama Salma Kikwete akipokewa kwa shangwe na wananchi wa mji wa Matai
waliofurika katika eneo la soko jipya mjini hapo ili kushiriki katika sherehe ya
kukabidhi pikipiki kumi kwa ajili ya watendaji wa vituo vya afya katika mikoa ya
Rukwa na Katavi tarehe 26.2.2013.
Mke wa Rais Mama Salma
Kikwete akimkabidhi funguo za pikipiki Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Katavi ambaye pia
ni Mkuu wa Wilaya ya Mpanda Ndugu Paza Mwamlima kwa ajili ya vituo vya afya vya
mkoa huo katika jitihada za kuzuia maambukizi ya virusi vya ukimwi kutoka kwa
mama kwenda kwa mtoto (PMTCT). Pikipiki hizo zimetolewa na kampuni ya
Waterrids.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete amembeba mtoto Emma, mwenye umri wa
miezi minne na nusu, mtoto wa Maria, ambaye alijeruhiwa kwa kukatwa mkono na
watu wasiojulikana wakati walipovamia nyumbani kwake tarehe 10.2.2013. Maria ni
mke wa tatu wa Bwana Gabriel Yohana ambaye siku ya tukio hakuwepo nyumbani kwa
Maria wakati watu hao walipomvamia.
Mbunge wa zamani wa Kwela Ndugu Chrisant Mzindakaya akishiriki
kucheza ngoma ya utamaduni ya kabila la Wafipa wakati Mke wa Rais Mama Salma
Kikwete alipotembelea hospitali ya Mkoa wa Rukwa kwa ajili ya kukabidhi vifaa
mbalimbali vya tiba vyenye thamani ya shilingi milioni mia
saba.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya
Wanawake na Maendeleo, Mama Salma Kikwete akimkabidhi Mganga Mkuu wa Mkoa wa
Rukwa Dr. John Gurisha vifaa mbalimbali vya tiba kwa ajili ya hospitali ya Mkoa
wa Rukwa tarehe 26.2.2013. Vifaa hivyo vimeletwa nchini na Taasisi ya WAMA kwa
kushirikiana na Kampuni ya Project C.U.R.E kutoka Marekani na vina thamani ya
shilingi milioni mia saba.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete hayupo pichani akiongea na wanafunzi
wa kike kutoka shule mbalimbali za sekondari katika Manispaa ya Sumbawanga
waliokusanyka katika shule ya sekondari ya Mtakatifu Theresia tarehe
26.2.2013
Post a Comment