MELI ya Mv Victoria
inayomilikiwa na Kampuni ya huduma za Meli nchini (MSC) imenusurika kuteketea
kwa moto uliozuka wakati mafundi wa kampuni hiyo wakichomelea eneo la shimo la
kuhifadhia mizigo la mojawapo ya maeneo kwenye Meli
hiyo
Moto huo uliozuka katika
meli hiyo ulizua tafrani kwa wakazi wa jiji la Mwanza na kufurika katika eneo la
maegesho ya Meli za Kampuni ya MSC yaliyopo katika bandari ya Mwanza kaskazini
majira ya saa 8 na dakika kadhaa na kusababisha msongamano mkubwa katika eneo
hilo.
Kwa mujibu wa taarifa
zilizo naswa toka kwa wafanyakazi wa Meli hiyo ambao hawakutoa ushirikiano
kuzungumza na waandishi wa habari, zilizonaswa wakati wakilaumiana zimeleeza
kuwa mafundi wa kampuni hiyo walikuwa wakichomelea katika moja ya vyumba vya
chini vya Meli hiyo ndipo cheche za moto zilipopenya na kuangukia katika sehemu
ya pili ya kuhifadhia mizigo na kuanza kuwaka.
Sehemu hiyo ya mizigo
kulikuwa kumehifadhiwa shehena ya magodoro pamoja na mito ya makochi tayari kwa
ajili ya kusafirishwa kwenda mjini Bukoba Mkoani Kagera leo
usiku.
Ni hali halisi ndani ya
Sehemu hiyo ya mizigo kulikuwa kumehifadhiwa magodoro pamoja na mito ya makochi
tayari kwa ajili ya kusafirishwa kwenda mjini Bukoba Mkoani Kagera leo
usiku.
Maafisa wa kikosi hicho
walijitosa kuhakikisha moto huo hausambai katika maeneo mengine ya Meli ya Mv
Victoria ambapo walifanikiwa kuuzima huku ukiwa tayari umeteketeza magodoro yote
pamoja na mito ya makochi iliyokuwa katika chumba cha kuhifadhia mizigo.Picha
kwa Hisani ya G sengo
Blog
Post a Comment