Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MKURUGENZI MKUU WA UNESCO AMALIZA ZIARA YAKE KWA KUKUTANA NA RAIS DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE

 

Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo ya Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Bi. Irina Bokova’s ( mwenye nguo ya blue) na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dkt. Alberic Kacou (wa katikati kushoto) wakibadilishana mawazo na ujumbe walioongozana nao kabla ya kukutana na Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam jana tarehe 5 February, 2013.
Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Bi. Irina Bokova’s akionekana kuvutiwa na moja ya picha za Tinga Tinga iliyopo chumba cha wageni Ikulu jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Bi.Irina Bokova’s akiwa ameongozana na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dkt. Alberic Kacou wakiingia sehemu maalum kwa ajili ya kuzungumza na Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Bi. Irina Bokova’s Ikulu jijini Dar es Salaam jana.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dkt. Alberic Kacou Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya ukumbusho na Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Bi. Irina Bokova’s alipotembelea na kufanya mazungumzo na Rais Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam jana.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Bi. Irina Bokova’s (wa tatu kushoto) na Ujumbe aliongozana nao kwa ajili ya mazungumzo na Rais Kikwete. Wa kwanza kulia ni Balozi wa Tanzania nchini Ufaransa Mh. Begum Taj, Mwakilishi wa Shirika la UNESCO nchini Tanzania Vibeke Jensen ( wa pili kulia), Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dkt. Alberic Kacou, Mkurugenzi Msaidizi wa UNESCO Afrika Bi. Lalla Aicha Ben Barka (wa pili kushoto) na wa kwanza kushoto ni Naibu Mkurugenzi wa UNESCO Bi. Robertine Raonimahari.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Bi. Irina Bokova’s Ikulu jijini Dar es Salaam jana.
Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Bi. Irina Bokova’s na ujumbe wake wakimsikiliza Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete (hayupo pichani) alipohitimisha ziara yake kwa kumtembelea Ikulu jijini Dar.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akipokea zawadi kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Bi. Irina Bokova’s aliyemtembelea Rais Kikwete Ikulu jijini Dar jana. Kushoto ni Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dkt. Alberic Kacou.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimsindikiza mgeni wake Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Bi. Irina Bokova’s aliyemaliza ziara yake ya kikazi ya siku mbili nchini baada ya kukutana na Rais Dkt. Kikwete Ikulu jijini Dar es Salaam jana tarehe 5, February, 2013.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimuaga Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO Bi. Irina Bokova’s aliyemtembelea Ikulu jijini Dar es Salaam jana jioni.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Dkt. Alberic Kacou Ikulu jijini Dar es Salaam jana jioni. (Picha zote na Zainul Mzige wa Mo Blog).
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top