Kikosi cha
Mtibwa.
Yanga na Mtibwa Sugar
zinapambana kesho (Februari 2 mwaka huu) katika moja ya mechi za Ligi Kuu ya
Vodacom. Mchezo huo utafanyika Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
Mwamuzi Ronald Swai kutoka
Arusha ndiye atakayechezesha mechi hiyo inayotarajiwa kuwa na upinzani mkali,
kwani wakati Yanga ikiongoza ligi hiyo, wapinzani wao Mtibwa Sugar katika mechi
iliyopita walilala mbele ya Polisi Morogoro ambayo ni ya mwisho katika msimamo
wa ligi kwa sasa.
Polisi Morogoro itakuwa
mwenyeji wa African Lyon kwenye Uwanja wa Jamhuri, mjini Morogoro wakati Uwanja
wa Mkwakwani, jijini Tanga utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Mgambo Shooting na
Ruvu Shooting inayofundishwa na Charles Boniface Mkwasa.
Keshokutwa (Jumapili)
kutakuwa na mechi mbili. Simba itaumana na JKT Ruvu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar
es Salaam huku Tanzania Prisons ikiikabili Coastal Union katika Uwanja wa
Mkwakwani jijini Tanga.
*LIGI DARAJA LA KWANZA,
VILLA SQUAD, MORO UNITED UWANJANI KESHO
Villa Squad na Moro United
zinaumana kesho (Februari 2 mwaka huu) Uwanja wa Karume, Dar es Salaam katika
moja ya mechi za kundi B za Ligi Daraja la Kwanza (FDL) inayoanza mzunguko wa
lala salama.
Kundi A litakuwa na mechi
kati ya Mbeya City na Burkina Faso itakayochezwa Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya,
Majimaji na Kurugenzi katika Uwanja wa Majimaji mjini Songea, na Polisi Iringa
dhidi ya Mkamba Rangers kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Samora mjini
Iringa.
Mechi nyingine ya Kundi B
itakuwa Transit Camp na Ndanda itakayochezwa Uwanja wa Mabatini mkoani Pwani.
Kundi C ni Polisi Dodoma na Kanembwa JKT (Uwanja wa Jamhuri, Dodoma), Morani
dhidi ya Mwadui (Uwanja wa Kiteto, Manyara), Polisi Mara na Pamba (Uwanja wa
Karume, Musoma), Polisi Tabora na Rhino Rangers (Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi,
Tabora).
Ligi hiyo inatarajiwa
kumalizika mwishoni mwa Machi mwaka huu ambapo mshindi wa kila kundi atapanda
daraja kucheza Ligi Kuu msimu
ujao.
Post a Comment