CHAMA cha NCCR-Mageuzi,
kimesema taifa limepoteza muelekeo kutokana na viongozi wake wengi waliopewa
dhamana ya kuongoza kushindwa kutimiza wajibu wao, hali ambayo imesababisha
wananchi kuishi katika mkanganyiko mkubwa.
Hayo yalisemwa jana, Jijini hapa na
Mjumbe wa Halmshauri Kuu taifa ya chama hicho, Juju Danda, katika tukio la
kuwapokea wanachama wapya 21 waliojunga na chama hicho, wakitokea Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Akizungumza katika mkutano huo uliofanyika
katika ukumbi wa hoteli ya Double J, mbele ya waandishi wa habari, Danda
alisema ili taifa liweze kupiga hatua za kimaendeleo ni lazima liwe na siasa
safi na uongozi bora.
Alisema kutokana na dhana hiyo kukosekana kwa viongozi
waliopewa dhamana ya kuongoza kumesababisha kuliacha taifa na wananchi wake
wakiishi katika mkanganyiko mkubwa unaotokana na kupanda kwa gharama za
maisha.
“Vyakula vimepanda, kadhalika nauli…. Kwa ujumla gharama za maisha
imepanda sana nahii yote imesababishwa na taifa kukosa watu wa kufanya siasa
safi ambazo zingetuletea viongozi bora” alifafanua Danda.
Alisema msingi pekee
wa taifa kupata maendeleo ni rasilimali watu ambayo imejengwa kwa kupewa elimu,
hivyo kitendo cha serikali ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kukosa mitaala ya elimu
ni inaonesha taifa lilivyokosa muelekeo.
“Rasilimali watu ni muhimu katika
mchakjato wa maendeleo kuzidi hata hayo madini, lakini umeona kilichotokea juzi
pale bungeni…. Mwenyekiti wetu (Jems Mbatia-NCCRA-Mageuzi) alichokieleza na
kilichotokea”.
Aliongeza kuwa licha ya CCM iliyoiweka serikali madarakani
kujipambanua kwa itikadi ya ujamaa na kujitegemea, lakini serikali hiyo
imeshindwa kuisimamia hivyo kufanya taifa kushindwa kujitegemea na badala yake
limegeuka kuwa ombaomba.
Alisema hali hiyo inajidhihirisha kwenye bajeti ya
serikali, kwani zaidi ya asilimia 40 ya bajeti hiyo inategemea msaada wa wafadhili
jambo linalokinzana na mfumo wa itikadi yake iliyojiwekea kama malengo wakati
ikitafuta dhamana ya kupewa nafasi ya kuongoza nchi.
Kwa upande wake mwakilishi
wa kundi la wanachama 21 waliohamia ndani ya NCCR-MAgeuzi, Moses Mwasubira,
ambaye alikuwa mwenezi wa Chadema wilaya ya Mbeya Mjini, alisema wamefikia
uamuzi huo kutokana na sababu mbalimbali.
Miongoni mwa sababu hizo ni kudai
kuwa uongozi wa taifa wa Chadema kushindwa kujenga Demokrasia ya kweli ndani ya
chama kwa kukumbatia ufisadi wa kutumia vibaya ruzuku ya chama na kuwaacha wa
mikoani wakifanya kazi kubwa ya kuchangisha fedha.
Uongozi mbaya wa Katibu Mkuu
wa chama hicho taifa,Dk.Willbroad Slaa na Mwenyekiti wake Freeman Mbowe,
kushindwa kusimamia katiba ya chama hicho katika kutatua migogoro, badala yake
wakitumia na kuamini kuwa kufukuza wanachama tena kwa majungu ndio suluhisho la
kukijenga na kukiimarisha chama.
Lakini pia walilalamikia chama hicho kujaa
utashi wa nguvu ya umma na kulazimisha maandamano, migomo vitu ambavyo si vya
lazima na kwamba kamwe hiyo si njia sahihi na malengo ya kweli ya kutafuta
ukombozi.
Naye mmoja wa kada Chadema, Emanuel Mwangoka (Cash Money), ambaye
inadaiwa kuwa ndiye alikuwa mfadhili Mkuu wa mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph
Mbilinyi (Chadema), akikabidhiwa kadi ya chama kipya, alisema atatumia uwezo
wake wote kama alivyofanya kwa sugu kuhakikisha NCCR-Mageuzi inaibuka na
kung’ara mkoani hapa.
Kwa upande wake aliyewahi kuwa Katibu wa Chadema Mkoa wa
Mbeya na kujiunga na NCCR-Mageuzi , Januari 20 mwaka huu Eddo Mwamalala,
alisema wanachama hao waliomfuata ni mtaji mkubwa wa kuhakikisha inakimaliza
chadema mkoani hapa.
Na Moses Ng’wat, Picha na Mbeya yetu
|
Post a Comment