Wizara ya Maji imesaini mikataba ya upanuzi wa miradi ya maji katika mikoa ya Kigoma, Lindi na Halmashauri ya mji wa Sumbawanga ,makubaliano hayo yaliyofanywa kati ya wizara na Wakandarasi watano.
Akisaini mikataba hiyo jana
Makao Makuu ya Wizara Ubungo , Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Mhandisi
Chistopher Sayi aliwataka wakandarasi hao kutekeleza miradi hiyo kwa wakati kama
mikataba inavyoeleza.
“Natumia nafasi hii
kupongeza wakandarasi wote walioshinda zabuni za kutekeleza miradi hii, lakini
pia ni mategemeo yangu miradi yote itafanywa kwa wakati kama ambavyo
tumekubaliana katika mikataba hii”. Alisema Mhandisi Sayi.
Wakandarasi waliopata
fursa ya kutekeleza ujenzi wa miradi hiyo ni Spencon Services Ltd ambao
watahusika na usambazaji na mifumo ya majisafi mkoani Kigoma; Jandu Plumbers na
Metito Overseas watahusika na uchimbaji wa visima katika Halmashauri ya mji wa
Sumbawanga.
Jandu Plumbers na Metito
Overseas watahusika na uchimbaji wa visima mkoani Lindi na Technofab-Gammon
Joint usambazaji na mifumo ya majisafi katika Halmashauri ya mji wa Sumbawanga,
na Overseas Infrastructure Alliance watahusika na usambazaji wa maji na mifumo
ya majisafi mkoani Lindi.
Miradi
hiyo ambayo itagharimu takriban shilingi bilioni 90 za kitanzania ambayo
imefadhiliwa na Jumuiya ya Umoja wa Ulaya Serikali ya
Ujerumani.
Post a Comment