Kambi Mbwana |
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
WAKAZI wa Dar es Salaam wenye asili
ya wilayani Handeni, mkoani Tanga, pamoja na maswahiba zao, wamepanga kukutana Ijumaa
ya Februari 8, katika Viwanja vya Leaders Club, kuanzia saa 10 za jioni ili
kutafuta namna ya kusaidia watu wasiojiweza wilayani humo.
Kikao hicho ni cha kwanza kufanywa
na watu wa asili ya Handeni, katika jiji hili ambalo wananchi wengine kutoka
mikoa na wilaya mbalimbali wamekuwa wakikutana na kujadili hali ya maisha
inayowakabili.
Akizungumza jana jijini Dar es
Salaam, mmoja wa wajumbe wanaoandaa kikao hicho, kilichopewa jina la ‘Handeni
Kwetu’, Kambi Mbwana, alisema kwamba kukutana kwa wadau hao ni sehemu maalum ya
kutafuta namna pia ya kusaidiana na viongozi wao kwa ajili ya maendeleo yao.
Alisema kwamba Wilaya ya Handeni
imekuwa ikikabiliwa na matatizo ya kila aina, ikiwamo njaa na shida ya maji,
hivyo kwa wananchi hao kukutana pamoja, wanaweza kupata ufumbuzi katika baadhi
ya mambo.
“Wakati Handeni ikiendelea kutajwa
kama wilaya zisizokuwa na maendeleo kwa miaka 51 ya Uhuru, sisi tunakutana na
kutoa kauli moja yenye tija kwa watu wote.
“Bila kuangalia nafasi zetu, vipato
vyetu au heshima katika jamii, naamini moyo tu wa kukaa na kuzungumza au kuimba
wimbo mmoja wa maendeleo, naamini mambo yatakuwa mazuri, hasa pale
kitakapofanyika kilichojadiliwa na wote,” alisema.
Post a Comment