|
MOJA
YA MTOTO MAJERUHI AKIHAMISHWA KUTOKA KATIKA HOSPITALI YA MISION CHIMARA NA
KUPELEKWA HOSPITALI YA RUFAA MBEYA |
|
MOJA
YA MAJERUHI AKISUBIRI KUPATA MATIBABU |
|
HILI
NDILO ROLI WALIMOPANDA VIBARUA HAO WA SHAMBA LA
KAPUNGA |
|
KWELI
MUNGU NI MKUU HUWALINDA WATOTO WADOGO HAPA MKUU WA MKOA AKIMPA MOJA YA WATOTO
WALIOPATA AJALI |
|
HUYU
BINTI NI MWANAFUNZI NAE ALIKUWEPO KWENYE AJALI
HIYO |
|
MKUU
WA MKOA MBEYA ABAS KANDORO AKIONGEA NA WAANDISHI WA
HABARI |
|
HAWA
WOTE NI WANAFUNZI WALIKUWA WANAENDA KUFANYA KIBARUA CHA KULIMA KWA MWEKEZAJI
KATIKA SHAMBA HILO LA KAPUNGA |
|
MAJERUHI
22 WAKIPAKIZWA KATIKA ROLI AINA YA FUSO TAYARI KUPELEKWA KATIKA HOSPITALI YA
RUFAA MBEYA |
|
MAJERUHI
WAKISAFIRISHWA KWENDA MBEYA |
|
MWANDISHI WETU JOSEPH MWAISANGO AKITOKA KATIKA HOSPITALI
YA CHIMALA BAADA YA KUSHUHUDIA NA KUPATA HABARI ZA UHAKIKA MAANA TAARIFA YA
AWALI ILITOLEWA KUWA WATU WASIOZIDI 30 WAHOFIWA KUFA KATIKA AJALI SASA
TUNAHABARI KAMILI BAADA YA MBEYA YETU KUFIKA KATIKA TUKIO
WATU watano
wamepoteza maisha na wengine 130 wamejuruhiwa vibaya huku hali zao zikiwa mbaya
baada ya Lori walilokuwa wakisafiria shambani kuacha njia na kupinduka katika
kijiji cha Mapogolo kata ya Itamboleo Wilayani Mbarali Mkoani
hapa.
Ajali hiyo
imetokea leo saa 1:30 asubuhi ambapo lori hilo ambalo ni mali ya Mwekezaji wa
shamba la Kapunga Rice Project, na kwamba watu hao walikuwa wakielekea kwenye
shamba la mwekezaji huyo lililkuwa limebeba vibarua hao zaidi ya 200 ambao ni
wakazi kitongoji cha Kapunga.
Lori hilo lenye namba za uasjili T398 BSE Scania Tipa,
ambalo lilikuwa likiendeshwa na dereva aliyejulikana kwa jina Baraka Moreli,
lilionekana likiwa katika mwendo kasi na dereva huyo akiwa na lengo la kutaka
kuipita pikipiki iliyokuwa mbele yake. huku akishangiliwa na vibarua hao ipite
ipite hiyo pikipiki haiwezi kutushinda sisi gari kubwa moja ya majeruhi alisema.
ndipo walipofika kwenye kona dereva lilimshinda gari hilo na
kupinduka
Akiwa
Hospitalini hapo Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro ambaye aliweza kufika
hospitalini hapo alisema kuwa mara baada ya kupata taarifa ya ajali hiyo kutoka
kwa Mkuu wa Wilaya ya ,Mbarali Gullam Hussein Kiffuu, huku akiombwa kupatiwa
msaada wa kuongezewa madaktari, kuongezewa vifaa vya mataibu sambamba na
uwezekano wa kupata damu kwa ajili ya kuwaongezea majeruhi hao alifanikiwa
kuwasiliana na uongozi wa hospitali ya Rufaa ya Mbeya, hospitali ya Mkoa ili
kuweza kuona namna ya kwenda kuokoa maisha watanzania hao.
Kandoro,
alisema kuwa katika ajali hiyo wanaume wanne wamefariki na mwanamke mmoja.
watatu wametambuliwa
Samweli
Mapugilo mbena 30 mkazi wa Ilembula
Bon Mfupa 27
mkazi wa mapogolo na Edgar Mwakipesile 35 mkazi wa Nonde Mbeya
Aidha, Kandoro alisema kuwa idadi ya majeruhi katika
ajali hiyo kuwa ni 130 ambapo wanawake ni 40 na wanaume 89 huku idadi ya watoto
waliokuwa wameongozana na wazazi wao haikuweza kufahamika kwa
haraka.
Pcha Mbeya
yetu
|
on Friday, February 1, 2013
Post a Comment