Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

WAZIRI WA MICHEZO MGENI RASMI KILIMANJARO MARATHONI


 

Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dkt Fenella Mukangara
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dkt Fenella Mukangara


WAZIRI wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk Fenella Mukangara anatarajiwa kufungua mbio za 11 za Kilimanjaro Marathon zitakazofanyika Jumapili hii mjini Moshi.
Mkurugenzi Mkuu wa Executive Solutions ambao ndiyo waratibu wa mbio hizo, Aggrey Marealle alithibitisha uwepo wa Waziri Mukangara siku hiyo na kueleza kuwa ndiye atazifungua mbio hizo sambamba na kutoa zawadi kwa washindi.
Tayari washiriki zaidi ya 6,000 kutoka nchi zaidi ya 40 wamethibitisha kushiriki kwenye mbio hizo zitakazofanyika katika makundi ya mbio ndefu za marathon (km 42), nusu marathoni (km21) na mbio za km 5 za kujifurahisha.
"Waziri Mukangara atashiriki pia katika hafla ya utoaji zawadi kwa washindi 10 bora wa mbio za km 42 (Kilimanjaro Premium Lager Marathon) kwa wanaume na wanawake,"alisema Marealle.
Kwa mujibu wa Marealle, mbali na Waziri Mukangara, viongozi mbalimbali wa Serikali akiwamo Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama watashiriki kwenye mbio hizo.
"Mbio za Kilimanjaro Marathon zinaiweka Tanzania kwenye ramani ya kimataifa kila mwaka, pia zinatoa fursa kwa wanariadha wa ndani kukua zaidi, kukuza utalii wa Tanzania na watu kupata nafasi ya kujenga afya zao," alisema Marealle.

Marealle alibainisha kuwa mbio hizo zitakuwa na hadhi ya kimataifa ambapo zitasimamiwa na klabu ya Kilimanjaro Marathon, Chama cha Riadha Tanzania (AT) na kile cha Mkoa wa Kilimanjaro.
"Ilikuhakikisha usalama wa wakimbiaji, baadhi ya barabara za ndani na nje ya mji wa Moshi zitafungwa kuanzia saa 12:15 asubuhi hadi 03:30 asubuhi siku hiyo kwa lengo la kuwapa fursa wakimbiaji kupita salama,"alisema Marealle.

Mbio hizo zinadhaminiwa na kampuni ya bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chao cha Kilimanjaro Premium Lager, Vodacom Tanzania (iliyodhamini mbio za Km 5 Fun Run), GAPCO (Nusu Marathon kwa Walemavu), Tanga Cement, CFAO Motors, KK Security, Keys Hotel, TPC Sugar, Tanzanite One, New Arusha Hotel, UNFPA, Fastjet na Kilimanjaro Water
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top