Mkuu wa Wilaya ya Temeke Sophia Mjema (kulia) akiongea katika halfa ya jioni katika maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Wanawake duniani iliyoandaliwa na benki ya Ecobank Tanzania Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Sophia Mjema (wa pili kulia) akiongea na Mwenyekiti wa Benki ya Ecobank, Rukia Mjema huku Mkurugenzi Mtendaji Enoch Osei-Safo (kulia) na Mkurugenzi wa Jumla wa Professional Approach Group Modesta Mahiga.
Mkuu wa Wilaya ya Temeke Sophia Mjema (kushoto) akialika wageni kusherekea kwa kugonganisha glasi. Wanaompongeza ni wafanyakazi waandamizi wa benki hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Ecobank Tanzania, Enoch Osei-Safo akiongea wakati wa hafla ya jioni katika maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Wanawake duniani iliyoandaliwa na benki hiyo Dar es Salaam juzi.
Baadhi ya wafanyankazi wa benki hiyo wakicheza katika hafla hiyo.
………………………………………………………
Ecobank Tanzania ambayo ni mojawapo ya benki katika kundi la Ecobank Afrika, leo inaadhimisha siku ya wanawake duniani katika sherehe iliyoandaliwa na benki hiyo ambapo mgeni rasmi alikuwa Mhe. Sophia Mjema, Mkuu wa Wilaya ya Temeke.
Sherehe hii ilifanyika kwa heshima ya wadau wote wanawake kutoka Ecobank na sekta ya benki nchini. Katika kuadhimisha mandhari ya siku hii “kupata kasi” Ecobank iko katika mstari wa mbele katika kuongeza kasi katika kukuza ushirikishwaji wa fedha kwa wanawake ambao wanalo jukumu muhimu sana katika kukuza uchumi wa Tanzania.
Bw. Enoch Osei-Safo Mkurugenzi wa Ecobank alisema, ‘tunatambua nafasi ya wanawake katika jamii yetu. Wanawake ndio kundi kubwa la wazalishaji wa chakula nchini, wafanyabiashara ndogondogo na za kati. Vilevile, wao ndio wanaotoa asilimia kubwa zaidi ya mapato yao katika kukuza familia na jamii. Wanawake wamechangia mno katika utoaji wa elimu kwa watoto na mahitaji ya msingi kwa jamii na hapo ili kuwawezasha zaidi, tulizindua upya akaunti ya watoto Pambazuka amabayo inawapa wazazi uwezo wa kuwawezasha wanao kusoma.’
Ecobank ina nia ya kuwawezesha watu na biashara Afrika ili kuwapa uwezo wa kupata mafanikio kutokana na rasilimali tulizo nazo hapa Afrika
Meneja mwajiri wa Ecobank Tanzania Bi. Maryam Mgeni alihakiki ahadi ya Ecobank katika kukuza nafasi ya wanawake katika jamii kwa kutambua thamani yao katika sehemu za kazi, na mchango wao wa kipekee nchini. ‘ Benki yetu imefaidika kutokana na ujuzi na maarifa ya wafanyakazi wetu wa kike. Kutoka kwa ngazi ya mwenyekiti wa bodi, wanawake wamechangia kwa kiasi kikubwa katika ukuaji wa benki yetu.’
Ecobank inazidi kusaidia wanawake Tanzania na Afrika kwa njia ya kupata huduma za kibenki kwa bei nafuu na kuchangia kupitia kushiriki kwetu kwenye harakati za kijamii.
Kwa habari zaidi, tafadhali tembelea: www.ecobank.com
Post a Comment