Mkurugenzi
wa Usalama na Ulinzi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema),
Wilfred Lwakatare akionesha ishara ya vidole ambayo ni salamu kwa
wafuasi wa chama chake wakati akiingia katika chumba cha Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.
Askari wa mbwa wakiimarisha ulinzi wakati wa kesi hiyo.
Mkurugenzi
wa Usalama na Ulinzi wa Chadema, Wilfred Lwakatare akiwa na mtuhumiwa
mwenzake, Ludovick Joseph wakiingia mahakamani leo.
Mkurugenzi wa Usalama na Ulinzi wa
Chadema, Wilfred Lwakatare akiwa na mtuhumiwa mwenzake, Ludovick Joseph
wakiingia mahakamani leo.
Polisi wakisindikiza msafara wa gari lililompakia Mkurugenzi wa Usalama
na Ulinzi wa Chadema, Wilfred Lwakatare kuelekea mahabusu hadi April 3
mwaka huu.
Mkurugenzi wa Usalama na Ulinzi
wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Wilfred Lwakatare akionesha
ishara ya vidole ambayo ni salamu kwa wafuasi wa chama chake wakati akiingia
katika chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe akiteta jambo na mke wa Mkurugenzi wa Usalama na Ulinzi wa Chama hicho, Wilfred Lwakatare.
Jengo la Mahakama ya Kisutu.
Wafuasi wa Chadema wakiwa wamekusanyika nje ya mahakama hiyo.Picha Kwa Hisani ya Habari Mseto Blog
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi
Kisutu Dar es Salaam imewafutia kesi ya makosa
ya
ugaidi Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo
(CHADEMA), Wilfred Lwakatare na Ludovick Joseph baada ya Mkurugenzi wa
Mashitaka( DPP), Dk Eliezer Feleshi kuwasilisha hati ya kuwafutia kesi hiyo
washitakiwa kwa sababu hana haja ya kuendelea nayo.
Sambamba
na hilo, DPP ilimfungulia kesi ya makosa ya ugaidi upya Lwakatare na Ludovick
ambapo kesi hiyo mpya namba Na.6/2013 ambapo imepangiwa kwa hakimu mpya Aloyce
Katemana.
Katika kesi ya ugaidi Na.37/2013 iliyofunguliwa na
Jamhuri dhidi ya Lwakatare na wenzake Machi 18 mwaka huu, ambayo ilifutwa saa
tatu asubuhi na ambayo ilikuwa imekuja kwa ajili ya Hakimu Mkazi, Emilius
Mchauru kuitolea uamuzi wa ama wa kuwapatia dhamana washitakiwa au la, hakimu
Mchauru alijikuta akishindwa kutoa uamuzi wake kwa sababu mawakili viongozi wa
serikali Ponsian Lukosi, Prudence Rweyongeza na Peter Mahugo waliwasilisha hati
hiyo ya DPP chini ya kifungu cha 91(1) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai
ya mwaka 2002, ambapo kifungu hicho kina mpa mamlaka DPP, kuifuta kesi yoyote ya
jinai muda wowote kabla ya haijatolewa hukumu na uamuzi huo wa DPP haujahojiwa
na mtu yoyote.
“Kwa kuwa kesi hii Na.37/2013 ilifunguliwa na upande
wa jamhuri MAchi 18 mwaka huu, na leo kesi hii ilikuja kwa ajili ya mahakama
kutolea uamuzi wa maombi ya washitakiwa kupatiwa dhamana au la pamoja na maombi
mengine…mahakama hii inasema haitaweza kutoa uamuzi wake kwa sababu DPP
amewasilisha hati ya kutotaka kuendelea kuwashitaki washitakiwa na hivyo
mahakama hii inawafutia kesi washitakiwa wote”alisema hakimu
Mchauru.
Baada ya hakimu Mchauru kuwafutia kesi, askari kanzu
waliwakamata tena washitakiwa hao na kuwaweka chini ya ulinzi wa gari la polisi
na ilipofika saa 4:20 asubuhi, washitakiwa hao wakiwa chini ya ulinzi mkali wa
wana usalama waliingizwa tena katika ukumbi namba mbili wa mahakama hiyo mbele
ya hakimu mkazi mwingine Aloyce Katemana.
Mawakili Wakuu wa Serikal, Ponsian Lukosi, Prudence
Rweyongeza na Wakili Mwanadamizi wa Serikali Peter Mahugo walidai kuwa kesi hiyo
nimpya na imepewa Na.6 ya maka huu, ambapo washitakiwa ni Lwakatare na Ludovick
wanaotetewa na mawakili wa kujitegemea Profesa Abdallah Safari na Peter Kibatara
na kwamba hati hiyo mashitaka ina jumla ya mashitaka manne ambapo shitaka la
kwanza linaangukia kwenye Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2002 na makosa
matatu yote yanaangukia kwenye Sheria ya Kuzuia Ugaidi ya mwaka
2002.
Wakili Rweyongeza alililata kosa la kwanza ambalo
linawakabili washitakiwa wote kuwa ni la kula njama kutenda kosa la jinai
kinyume na kifungu cha 284 cha Sheria ya Kanuni ya Adhabu ya mwaka 2002 , na
kwamba mnamo Desemba 28 mwaka jana, huko Kimara King’ong’o Stopover, wote kwa
pamoja walitenda kosa hilo kwa kutaka kutumia sumu kwa lengo la kumdhuru Denis
Msaki ambaye ni Mhariri wa habari wa Gazeti la Mwananchi ambalo ni kinyume na
kifungu cha 227 cha sheria hiyo.
Wakili Rweyongeza alilitaja kosa la pili kuwa ni la
kula njama ambalo pia ni kwaajili ya washitakiwa wote ambalo ni kinyume na
kifungu cha 24(2) cha Sheria ya Kuzuia Ugaidi Na.21 ya mwaka 2002, ambapo
washitakiwa hao walitenda kosa la ugaidi la kutaka kumteka Msaki kinyume na
kifungu cha 4(2)(c) (iii) cha Sheria ya Kuzuia Ugaidi ya mwaka
2002.
Shitaka la tatu ni la washitakiwa wote ambapo
wanashitakiwa kwa kosa la kupanga kufanya makosa ya ugaidi kinyume na kifungu
cha 59(a) cha Sheria ya Kuzuia ugaidi kwamba Desemba 28 mwaka jana,walishiriki
katika mkutano wa kupanga kufanya vitendo vya kumteka nyaraka Msaki kinyume na
kifungu 4(2)(c) (iii) cha Sheria ya Kuzuia Ugaidi.
Shitaka la nne, Rweyongeza alidai linamkabili
Lwakatare peke yake ni kuwezesha kutendeka kwa kosa la ugaidi kinyume na
kifungu cha 23(a) cha sheria ya kuzuia ugaidi , kwamba Desemba 28 mwaka jana,
Lwakatare akiwa ni mmiliki nyumba hiyo ilipo Kimaraka King’ong’o kwa makusudi
aliliruhusu kufanyika kwa kikao hicho baina yake na Ludovick cha kutenda kosa
la ugaidi la kutaka kumteka nyara Msaki hata hivyo walikanusha mashitaka
hayo.
Hata hivyo Hakimu Katemana alisema washitakiwa hao
hawatakiwi kujibu chochote kwasababu mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza
kesi hiyo na akaiarisha kesi hiyo hadi Aprili 3 mwaka huu, itakapokuja kwa ajili
ya kutajwa.
Wakili Kibatala aliomba mahakama isikilize ombi lake
alilokuwa akitaka kuliwasilisha, lakini Hakimu Katemana alisema yeye ndiye
kiongozi na mawakili wa utetezi, Jamhuri wapo chini yake na akamweleza Kibatala
mahakama ni mhimili unaongozwa kwa taratibu zake na nilazima Kibatala azifuate,
hivyo, kwa kuwa yeye hakimu ana majukumu mengine, leo hayupo tayari kusikiliza
ombi la Kibatala wala ombi la upande wa Jamhuri (lilokuwa linaomba mahakama
imruhusu Ludovick aendelee kushikiliwa na jeshi la polisi kwa ajili ya hatua
zaidi za kipelelezi,) na kuamuru washitakiwa wapelekwe
gerezani.
Itakumbukwa kuwa Machi 18 mwaka huu, Hakimu Mchauri
alitoa fursa kwa washitakiwa ya kukubali au kukanusha mashitaka licha ya Hakimu
wa Mahakama hiyo ya Hakimu Mkazi kutokuwa na ruhusa ya kutoa fursa hiyo
kulingana na makosa yanayowakabili watuhumiwa na kwa mujibu wa sheria za nchi.
Mahakama Kuu pekee ndiyo yenye mamlaka ya kusikiliza kesi za makosa ya tuhuma
za ugaidi.
Baada ya kesi hiyo kuairishwa wafuasi wa CHADEMA na
watu wengine wakiwa wamevalia sare walipaza sauti na kusema ‘Peoples Power…
hakuna kulala hadi kwanza walale wao’.
Hali iliyosababisha wanausalama waliokuwa wamevalia
sare na wale waliovalia kiraia waliokuwa ndani ya kumbi wa kesi ilipokuwa
ikiendeshewa kuwataka watu wote watoke ndani ya ukumbi huo haraka ili waweze
kuwapitisha washitakiwa, amri ambayo wafuasi hao waliitii bila
shuruti.
Msafara wa magari nane ukiongozwa na magari ya jeshi
la magereza, polisi waliondoka ndani ya viwanja hivyo kwa ajili ya kuwapeleka
watuhumiwa katika gereza la Keko , huku askari wa kikosi cha mbwa wakiwa bado
katika eneo la mahakama hiyo kwa ajili ya kuimarisha ulinzi. Hata hivyo, hali
ilikuwa ni shwari kwa sababu hakukuwepo na vitendo vya uvunjifu wa amani kwani
wafuasi wa CHADEMA waliondoka mahakamani hapo kwa utulivu wa hali ya juu huku
wengine wakiangua vilio kwa uchungu.
Mbwa waliokuwepo wakiimarisha ulinzi eneo hilo ni
Kino, Pd Kambi Simba, Giro, Pd Roja, Pd Ivo, Pd Undra, Pd Bobi ambao wamepata
mafunzo ya kuimarisha ulinzi kutoka nchi mbalimbali ikiwemo
Lebanon.
Akizungumza nje ya viwanja vya mahakama baada ya
kesi kuahirishwa, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe alisema kwanza
asingependa kuingilia mtiririko wa mahakama na kuwataka waandishi wa habari
wamuhoji wakili wa washitakiwa.
Akasema wao wanafanyakazi za mageuzi kwa ajili ya
kuwatetea raia wanyonge na maskini na kwamba kilichompata Lwakatare siyo geni,
bali ni mtiririko wa mabavu ya dola dhidi ya wanamageuzi.SOURCE
MPEKUZI
Post a Comment