IGP SAIDI
MWEMA.
Dk Ulimboka kabla hajaanza
kutibiwa.
Mwenyekiti wa Jukwaa la
Wahariri, Absalom Kibanda.
MKUU wa
Jeshi la Polisi nchini (IGP), Said Mwema amesema upelelezi wa kesi ya kutekwa,
kuteswa na kutupwa katika msitu wa Mabwepande, Mwenyekiti wa Jumuiya ya
Madaktari Tanzania, Dk. Steven Ulimboka bado haujakamilika.
Mbali na Dk. Ulimboka, IGP alisema kesi nyingine zote
za aina hiyo pamoja na za mauaji ya watu mbalimbali, akiwemo Padri wa Kanisa
Katoliki la Minara Miwili lililopo Mji Mkongwe Zanzibar, Evaristus Mushi (56),
uchunguzi wake unaendelea.
IGP Mwema, aliyasema hayo jana wakati wa semina ya
wakuu wa Upelelezi wa makosa ya Jinai wa nchi za Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa
Afrika (SADC), Mjini Dar es Salaam jana.
Dk. Ulimboka ambaye ni Mwenyekiti wa Jumuiya ya
Madaktari Tanzania, alitekwa usiku wa kuamkia Juni 27,
2012.
Hata hivyo, suala hilo lilizua sintofahamu ya aina
yake baada ya mtuhumiwa Joshua Mulundi, raia wa Kenya kukamatwa na kufunguliwa
kesi, akishtakiwa kwa kosa la kumteka na kumtesa Dk.
Ulimboka.
Akijibu maswali mbalimbali ya waandishi wa habari
waliotaka kujua upelelezi wa kesi hiyo umefikia wapi, licha ya kukamatwa kwa
mtuhumiwa wa kesi hiyo, ambaye anaendelea kusota gerezani, IGP Mwema alisema
upelelezi wa kesi unategemea kupatikana mapema kwa ushahidi husika, vinginevyo
kesi za aina hiyo zinaweza kuchukua muda mrefu.
Hata hivyo, suala la mtu kufunguliwa kesi huku
akiendelea kusota rumande, limezua sintofahamu ya aina yake, huku watu wakihoji
upelelezi wa polisi kuchukua muda mrefu bila kukamilika, kwamba ni kumnyima haki
mshtakiwa.
Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Tanzania, Thomas Mihayo
alipotakiwa kuzungumzia hali hiyo, alisema dhamana ni haki ya mshtakiwa hivyo si
vema mtu kunyimwa dhamana bila sababu.
Hata hivyo, alisema si kila kosa linaweza kuwa na
dhamana na kwamba, hilo linategemea aina ya kosa
husika.
“Makosa yanayozuia kuwa na dhamana ni yale ya jinai,
lakini katika nchi zilizoendelea hata kama ni jinai lazima kwanza upelelezi
ufanyike kabla ya kumkamata mtuhumiwa, vinginevyo ni kinyume cha
utaratibu.
“Hapa kuna mambo mawili yanaweza kufanyika, upelelezi
lazima kwanza ukamilike ndipo akamatwe mtuhumiwa, lakini pia wanaweza kumkamata
mtuhumiwa, halafu akaachiwa kwa dhamana na upelelezi ukaendelea kufanyika ingawa
hapa kwetu yote hayafanyiki,” alisema Jaji Mihayo.
Kuhusu suala la Ulimboka, alisema mtuhumiwa huyo raia
wa Kenya, ameendelea kusota rumande kwa sababu ya kukosa wanasheria wa
kumsimamia na kuhakikisha haki inatendeka.
Alisema kama Mlundi, angekuwa na wanasheria
wangemsaidia kuonyesha ile kesi si halisia.
Alisema wakati mwingine kile kinachoitwa mada huwa
hakipo, kwa lugha ya kisheria zinaitwa ‘murder toy’, hivyo kesi za aina hiyo
wanasheria huzikatia rufaa kutokana na mazingira
yaliyopo.
Mbali na hoja hizo za kisheria, kwa nyakati tofauti,
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleimani Kova aliwahi kusema
suala la Ulimboka limefungwa na limebaki mikononi mwa uongozi wa juu wa jeshi
hilo.
Pia Msemaji wa jeshi hilo, Advera Senso alisema suala
la Dk. Ulimboka, limefungwa kwa sababu tayari liko
mahakamani.
Sakata hilo la Dk. Ulimboka liliendelea kuwa mwiba
mkali, baada ya baadhi ya vyombo vya habari pamoja na Ulimboka mwenyewe kumtaja
mtu mmoja, Rama Ighondu mmoja wa wafanyakazi wa Ikulu kuwa ndiye alihusika
kumteka.http://www.mtanzania.co.tz
Post a Comment