WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi, amesema Jeshi la polisi limewasimamisha kazi, na
kuwafungulia mashtaka ya kijeshi askari wake katika maeneo mbalimbali nchini kwa
kwenda kinyume na kanuni za kijeshi.
Akizungumza na waandishi wa
habari jijini Dar es Salaam jana, Dk Nchimbi, alisema katika kikao cha Maofisa
na Makamishna wa polisi kilichoketi Dodoma havi karibuni waliazimia kuanza
kuchukua hatua za kinidhamu kwa askari wote watakaokwenda kinyume na kanuni na
maadili ya jeshi hilo.
Nchimbi aliwataja
waliosimamishwa na kufunguliwa makosa ya kijeshi ni pamoja na Elis Mwita,
Mrakibu Mwandamizi wa Polisi ambaye alikuwa Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Mbeya,
Jacob Kiango, Mrakibu msaidizi wa Polisi, aliyekuwa msaidizi wa Mkuu wa
Upelelezi Mkoa wa Mbeya, na Charles Kinyongo mrakibu msaidizi wa Polisi ambaye
alikuwa mkuu wa kikosi cha kutuza ghasia Mkoa wa Mbeya.
Dk Nchimbi alisema askari
hao wote wanatuhumiwa kushiriki mchakato wa kutunza na kusafirisha mihadarati
aina ya cocaine, yenye uzito wa kilo 1.9, yaliyokamatwa katika kituo cha
Tunduma, kuthibitishwa na Maofisa wa Malaka ya Mapato (TRA), kuwa kweli ilikuwa
ni mihadarati.
Alisema lakini
walipoyaleta kwa Mkemia Mkuu wa Serikali, Dar es Salaam, na kufanyiwa chunguzi
ikabainika kuwa haikuwa mihadarati bali ilikuwa ni Chumvi na
sukari.
Dk Nchimbi alisema baada ya
taarifa hiyo Kamati ya Mkoa wa Mbeya ikaomba ifanyiwe uchunguzi na kubaini kuwa
kilichopelekwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali sicho kilichokamatwa, bali kulikuwa
na udanganyifu, jambo lililosababisha wizara iunde tume iliyobaini kuwa wana
tuhuma ya kujibu.
“Askari wadogo
wakishirikiana na maofisa wa TRA waliokamata mihadarati hiyo wanajua chumvi na
sukari, hivyo vigogo hao walishiriki katika njama ya kubadilisha”alisema DK
Nchimbi.
Akizungumzaia mgogoro wa
Ardhi kati ya mwekezaji na wanakijiji, Dk Nchimbi alimtaja Mrakibu Mwandamizi wa
Polisi, Peter Mtagi, kuwa amesimamishwa kazi na kufunguliwa mashtaka ya
kijeshi.
Alisema Mtagi ambaye pia
alikuwa Mkuu wa Upelelezi wa Mkoa wa Kagera anatuhumiwa kuwabambikizia kesi
wananchi kuwa majambazi, waliiba kwa kutumia silaha ili wasipatiwe dhamana baada
ya kupokea rushwa.
“Mimi sipendi watu wafanye
vurugu lakini napenda haki itendeke sasa katika hili askari hawa hawakufuata
taratibu na walikuwa wanajua kuwa wananchi wale walifanyavile baada ya kufanya
mkutano wa hadhara na kubaini kuwa mwekezaji yule hakuwa na haki ya kumiliki
ardhi kiasi hekari 4000”alisema.
Dk Nchimbi alisema wakati
wananchi hao wakiwaswaga ng’ombe kuwapeleka kwa Mkuu wa wilaya, lakini wakiwa
njiani walikamatwa na polisi, na wengine walikimbilia Dodoma kuonana na waziri
mwenyewe.
Alisema lakini wakiwa
huko, alipigiwa simu na askari polisi kutoka Kagera na kuelezwa kuwa watu hao ni
majambazi sugu, hata hivyo, Nchimbi aliomba akutane nao, baini kuwa wananchi hao
hawajawahi kuwa majambazi hivyo walisingiziwa tuhuma hizo kwa
makusudi.
Naye Mkuu wa Kituo cha
Polisi wa wilaya ya Serengeti, Paul Mng’ong’o (SSP), amefukuzwa kazi baada ya
kuingia katika Hifadhi ya Mbuga ya Wanyama Serengeti na kupanga njama ya
kuchimba madini aina ya dhahabu kinyume cha sheria, ambapo hivi sasa
amefunguliwa kesi.
Kwa upande mwingine Dk
Nchimbi alisema suala Kamishna Msaidizi Mwandamizi Renatus Chalamila, ambaye
alikuwa anasimamia ajira za jeshi la polisi, anatuhumiwa kwa pamoja na maofisa
wa polisi kujihusisha na vitendo kupokea rushwa na kuwaingiza vijana wengi
katika Chuo cha polisi kilichopo Moshi, kinyume cha
utaratibu.
“Katika tukio hili vijana
95 ambao waliingizwa katika chuo hicho cha askari bila ya kufuata utaratibu
tumechukulia hatua za kuwafukuza chuoni hapo”alisema Dk
Nchimbi
Nchimbi alisema kutokana na
cheo chaka hicho mwenye madaraka ya kumfukuza kazi ni Rais hvyo taarifa hizo
zomefikishwa kwenye mamlaka hiyo ambapo wakati wakisubiri maamuzi mengine
wanawajibika kumpa likizo ya mwzi mmoja.
Katika hatua nyingine Dk
Nchimbi alisema hawezi kuzungumziwa matukio ya kutekwa na kuteswa kwa Mwenyekiti
wa Chama cha Dk Stephen Ulimboka na tuhuma zinazowakabili polisi kukwapua fuko
lililokwa na sh milion 150 wakati wakitaka kuzima tukio la ujambazi eneo la
Kariakoo mwaka jana, Nchimbi alisema, “hayo ni masuala ambayo bado yako ngazi ya
chini mnaweza kumuuliza Kova, sio lazima yajibiwe na Waziri endapo atashindwa
kufanya hivyo basi nitawajibika
kujibu”
Post a Comment