Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na
Ushirikiano wa Kimataifa, Bw. John Haule (kulia) kwa pamoja na Balozi wa India
hapa nchini, Mhe. Debnath Shaw wakisaini Mkataba wa Makubaliano ya Ushirikiano
(MoU) kati ya Chuo cha Diplomasia (CFR) cha Tanzania na Taasisi ya Utamaduni ya
India (ICWA). Uwekaji saini huo ulifanyika Wizarani jana tarehe 19 Machi,
2013.
Bw. Haule akibadilishana Mkataba na Balozi Shaw
mara baada ya kusaini.
Katibu Mkuu Bw. Haule akizungumza na Balozi Shaw
mara baada ya kukamilisha zoezi la uwekaji saini mkataba wa Ushirikiano kati ya
Chuo cha Diplomasia cha Tanzania na Taasisi ya Utamaduni ya
India.
Mhe. Balozi Shaw akichangia hoja wakati wa
mazungumzo na Bw. Haule huku wajumbe wengine
wakisikiliza.
Mkurugenzi wa Chuo cha Diplomasia, Balozi
Mohammed Maundi (kushoto) pamoja na Mkurugenzi wa Idara ya Asia na Australasia
katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Balozi Mbelwa
Kairukiwakishuhudia uwekaji saini wa mkataba huo.
Wajumbe wengine waliohudhuria katika tukio hilo
la uwekaji saini wa mkataba. Kutoka kushoto ni Afisa kutoka Ubalozi wa India
hapa nchini, Bw. Gobal Krisha na Bw. Ali Ubwa, Afisa Mambo ya Nje kutoka
Kitengo cha Sheria.Picha Zote na Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano Wa
Kimataifa
Post a Comment