Meneja wa bia ya Kilimanjaro Bw. George Kavishe akizungumza na waandishi wa habari katika ofisi za TBL Masaki wakati alipozungumzia uzinduzi wa Tuzo za Kilimanjaro Music Award na kuasiniwa kawa mkataba wa udhamini wa Tuzo hizo kati ya kampuni ya TBL na BASATA.Kushilla Thomas Mkurugenzi wa Masoko wa TBL akibadilishana hati na Godfrey Mngereza Kaimu Katibu Mtendaji wa BASATA baada ya kusainiwa kwa mkataba huo, huku viongozi wengi9ne wa TBL na BASATA wakipiga makofi.
Katikati ni Kushilla
Thomas Mkurugenzi wa Masoko wa TBL kulia na Godfrey Mngereza Kaimu Katibu
Mtendaji wa BASATA kushoto pamoja na Maofisa wa TBL na BASATA
wakifurahia jambo mara baada ya kuzinduliwa rasmi kwa nembo ya Kilimanjaro
Music Award.
Tuzo za muziki maarufu kama
Kilimanjaro Tanzania Music Awards 2013 zimezinduliwa leo jijini Dar es Salaam
zikiwa na dhumuni kubwa la kutambua wasaniii waliopata mafanikio katika sekta ya
muziki kwa kipindi cha mwaka mmoja uliopita.
George Kavishe, Meneja wa
kinywaji cha Kilimanjaro Premium Lager amesema wakati wa uzinduzi huo kuwa,
“Kilimanjaro Premium Lager inajivunia kuendelea kudhamini tuzo hizi kwa mara ya
12 sasa lengo likiwa kukuza muziki nchini Tanzania. Mchakato wa kuwapata
wanamuziki bora wa mwaka unaanza leo na utamalizika tarehe 8 Juni ambapo
tutakuwa na hafla ya usiku maalum wa kwa ajili ya kutangaza
washindi.”
Alisema Kilimanjaro
Premium Lager imejizatiti kuendeleza tasnia ya muziki Tanzania kwa kutambua na
kuwapa tuzo wasanii wenye vipaji. ‘Tunataka wanamuziki wetu wajisikie
wanathaminiwa na kutambuliwa kwa kazi nzuri wanayoifanya vile vile tunataka
Watanzania waweze kuthamini muziki wa nyumbani na kutambua mchango wa
wanamuziki katika kuleta maendeleo ya uchumi katika nchi.
‘’Kilimanjaro Premium Lager
inajivunia kuwa sehemu ya tuzo hizi na ni matumaini yetu kua mwaka huu tukio
hili litakua kubwa na zuri zaidi’’
‘’Pia tuna furaha
kutangaza kwamba BASATA imetupatia leseni ya kuendelea kudhamini tuzo hizi kwa
kipindi cha miaka mingine mitano. Kusainiwa kwa mkataba mpya na BASATA ni
uthibitisho wa azma kubwa tuliyonayo katika kuendeleza muziki wa Tanzania.
Mkataba huu utaifanya Kilimanjaro Premium Lager kuwa mdhamini wa tuzo hizi mpaka
mwaka 2018
Post a Comment