Waziri mkuu aliyejiuzulu
Edward Lowassa amefanikisha kukusanywa kwa Sh85 milioni katika harambee ya
kukusanya fedha kwa ajili ya kutatua tatizo la ajira kwa vijana, mkoani
Arusha.
Harambee hiyo
iliyofanyika juzi, iliandaliwa na Umoja wa Waendesha Pikipiki (Uwapa) wa Jiji la
Arusha.
Akizungumza
katika harambee hiyo, Lowasa ambaye pia ni
Mbunge wa Monduli, aliwataka vijana kujiepusha na
ushawishi wa wanasiasa wanaowarubuni ili kushiriki katika maandamano yasiyokuwa
na tija.
Badala yake, aliwataka
wajikite katika kuzungumzia maendeleo yao. Alisema fedha zilizopatikana katika
tukio hilo, ni vyema zikatumika katika kukopeshana ili kupanua mitaji ya
biashara zao
Post a Comment