Miss World Africa 2005,
Nancy Sumari leo amezindua kitabu chake cha watoto kiitwacho Nyota Yako.
Uzinduzi huo umefanyika jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na watu mbalimbali
maarufu wakiwemo mamiss Tanzania wa zamani, Jacqueline Ntuyabaliwe na Faraja
Nyalandu.
Nancy Sumari akizungumza kwenye uzinduzi huo
Wengine ni pamoja DAKTARI
Bingwa wa magonjwa ya watoto na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya
Hubert Kairuki, Profesa Esther Mwaikambo, Jokate Mwegelo, Shaa, Ally Remtullah.
Fina Mango na wanafunzi mbalimbali.
Akizungumzia jambo
lililomsukuma kuandi ka kitabu hicho, Nancy
alisema:
Vilinisukuma vitu vingi,
kwanza nafasi ya mwanamke kwenye jamii yetu, umuhimu wake, sababu ya kumuenzi na
kumsherehekea na kutambua michango yetu, mwanamke mdogo, msichana mdogo, mama
zetu, bibi zetu. Kuna kila sababu ya sisi kuangaliana na kutambuana na pia
kufananisha.
Profesa Mwaikambo akikielezea kitabu hicho
Profesa Mwaikambo akimuonesha picha ya kwenye kitabu hicho mtoto wa
Nancy, Zuri
Sababu baada ya kutembea
kwenye shule nyingi na kuzungumza na wasichana wengi nimegundua kwamba story
zetu zinafanana. Changamoto ni nyingi tunazozipitia na tunafanana kwa vitu vingi
kwahiyo nikaona ni vyema nikawafananisha wasichana wengi wakamwangalia mwanamke
kama Dokta Migiro wakasikiliza story yake, wakajiona kwenye hiyo hadithi,
wakaona uwezo wao wa kufikia alipofikia Dokta Migiro.
K-Lyinn akisaini kitabu cha
waliohudhuria uzinduzi huo
Post a Comment