Ndugu zangu,
Na ikafika siku ya mikate isiyotiwa chachu. Siku hiyo Mwana- Kondoo wa Pasaka huchinjwa. Yesu akawatuma Petro na Yohana, akawaagiza; `` E nendeni mkatuandalie chakula cha Pasaka.”
Nao wakamwuliza; ``Tukaandae wapi?''
Yesu akawajibu; ``Mtakapokuwa mnaingia mjini, mtakutana na mwanaume aliyebeba mtungi wa maji. Mfuateni huyo huyo, mpaka kwenye nyumba atakayoingia.”
“Kisha mwambieni mwenye nyumba; Mwalimu anauliza, kiko wapi chumba cha wageni, ambamo mimi na wanafunzi wangu tutakula Pasaka? Atawaonyesha chumba kikubwa ghorofani. Chumba kilicho na fanicha zote. Fanyeni maandalizi humo.''
Basi, wakaenda, wakakuta kila kitu kama Yesu alivyokuwa amewaambia. Hivyo, wakaandaa chakula cha Pasaka. Wakati ulipofika, Yesu akaketi mezani pamoja na wanafunzi wake kumi na wawili. Kisha akawaambia;
``Nimetamani mno kuila Pasaka hii pamoja nanyi kabla ya kuteswa kwangu. Kwa maana, nawaambieni, hii ni mara yangu ya mwisho kula Pasaka mpaka maana halisi ya Pasaka itakapokamilika katika Ufalme wa Mungu.''
Hapo Yesu akapokea kikombe cha divai, akashukuru akisema, ``Chukueni mnywe wote. Kwa maana, nawaambieni, tangu sasa sitakunywa tena divai hadi Ufalme wa Mungu utakapokuja.'' Alitamka Yesu.
Ni Neno La Leo.
Nawatakia nyote Pasaka Njema!
Maggid,
Iringa
http://mjengwablog.co.tz
Post a Comment