GENGE HATARI LAIBUKA, CCM, CHADEMA VYAHUSISHWA.
Dk Steven Ulimboka akiwa chumba cha wagonjwa mahututi
MOI.
Mhariri Mtendaji Mkuu wa
Kampuni ya New Habari (2006) Limited, Absalom Kibanda, akiwa ndani ya Ndege ya
Flightlink.
Daudi Mwangosi
aliyekuwa mwandishi wa chanel ten akisulubiwa na askari polisi na kumfyatulia
bomu la machozi mwilini na kupoteza maisha mkoani Iringa. Mkurugenzi Mtendaji wa Hali halisi
publishers Ltd, Saed Kubenea akiwa katika wodi ya Hospitali ya Apollo, New
Delhinchi INDIA mara baada ya kufanyiwa Upasuaji macho, Kubenea amekuwa akitibiwa katika
Hospitali hiyo tokea mwaka 2008 alipomwagiwa tindikali katika ofisi yake jijini
Dar es Salaam na hii ni operesheni yake ya tano.
SASA ni dhahiri kwamba,
makundi yanayohasimiana ndani ya vyama vikuu vya siasa kwa sababu ya kusaka ukuu
wa dola mwaka 2015, yako tayari kufanya jambo lolote kuhakikisha yanafanikisha
malengo ya kuupata urais baada ya rais wa sasa, Jakaya Kikwete, kumaliza muda
wake, MTANZANIA Jumatano linaripoti.
Mlolongo wa matukio ya utekaji, utesaji na
mauaji ya watu maarufu hapa nchini ambayo yamekuwa yakihusishwa na makundi ya
watu wanaousaka urais, ni ushahidi tosha kwamba, makundi hayo yako tayari
kuingia Ikulu si kwa kutumia nguvu ya fedha tu, bali hata kwa kufanya jambo
lolote ambalo litahakikisha ushindi wao.
Wachambuzi na wafuatiliaji wa masuala ya
kisiasa wa hapa nchini wanayatafsiri matukio ya sasa ya uhalifu dhidi ya
binadamu kuwa ni mkakati unaoratibiwa kwa karibu na makundi yanayowania urais
mwaka 2015 ndani na nje ya Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Kwamba,
ndani na nje ya CCM, vita ya kisiasa baina ya makundi hasimu imekuwa kubwa kwa
kiwango cha baadhi ya wanasiasa kuwa na fikra za kuangamizana na ama kupeana
vilema vya maisha, ili kutimiza ndoto ya kuukwaa urais.
Kwa
upande mwingine, nje ya CCM, Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) ambacho
kwa muda mrefu kimekuwa kikinyooshewa kidole na CCM kwa kuendesha siasa za
kibabe zinazogharimu maisha ya Watanzania, nacho sasa kinakabiliwa na vita ya
makundi yanayowindana kuwania urais mwaka 2015.
Ni
mwenendo huo wa siasa za ndani uliosababisha mgawanyiko kwa wafanyakazi wa Idara
ya Usalama wa Taifa, ambako uchunguzi unaonyesha kuwa baadhi yao wameasi na
kuamua kufanya kazi kwa karibu na makundi yanayowania urais, badala ya ile ya
kusimamia maslahi ya taifa.
Vyanzo
vya habari kutoka ndani ya makundi hayo, vinaeleza kuwa matukio ya sasa ya
kudhuru watu maarufu yanadaiwa kufanywa na watumishi wenye mafunzo ya kutesa na
kuua walio ndani ya Idara ya Usalama wa Taifa kwa malengo yenye maslahi fulani
fulani.
Mmoja
wa wanasiasa maarufu hapa nchini ambaye amepata kushika nyadhifa mbalimbali
serikalini, amelieleza MTANZANIA Jumatano kuwa vitendo vya kushambulia na
kudhuru raia vinafanywa na watumishi wa Idara ya Usalama walioviasisi kwa
madhumuni ya kuwachonganisha wananchi na serikali yao, ili wazidi kujenga chuki
na watawala.
Anaeleza zaidi kuwa wanausalama wanaodaiwa
kuasi kutokana na kukatishwa tamaa na mwenendo wa uendeshaji serikali sasa
wamejipenyeza na kuwa wakala wa moja ya kundi la wanaCCM linalopambana na
makundi mengine ya ndani ya chama hicho kushika ukuu wa dola na wapo pia
wanaodaiwa kujipenyeza katika vyama vya upinzani, hususani Chadema na kushiriki
harakati za kuiondoa CCM madarakani.
Habari
zinadai kuwa ndani ya CCM wanausalama waasi wamekuwa wakitumiwa na baadhi ya
makundi hayo kutekeleza azma yao, ikiwa ni pamoja na kutekeleza mpango wa
kuumiza watu wenye ushawishi kwa jamii ambao mwenendo wao una athari mbaya kwa
makundi hayo.
Mkakati
unaotajwa wa kuwatumia waasi hao ni kuhakikisha wanadhoofisha makundi mengine
ambayo ni kikwazo kwao kwa staili ya kutoa vitisho, kupanga mipango ya kuteka
watu na kujeruhi.
Duru za
habari zimeeleza kuwa hatua ya Chadema kudaiwa kuhusika katika mipango ya
utekaji na utesaji wa watu mbalimbali, wakiwemo waandishi wa habari, ni mkakati
unaoratibiwa na maofisa usalama wa taifa walioasi, wanaotumiwa sasa na wapinzani
na baadhi ya makundi ya wanaCCM.
Kwamba
mkakati huo, unaratibiwa kwa malengo mawili tofauti, la kwanza likitajwa kuwa
ama Chadema wanashirikiana na watu hao kupanga vitendo hivyo ili kujenga chuki
baina ya serikali iliyoko madarakani na wananchi au kundi la wanaCCM
linalopambana chini ya kivuli cha kuilinda serikali, lakini likiwa na nia ya
kuichafua ili kufanikisha lengo lake la kushika dola.
Hoja
hii inajengwa na wafuatiliaji wa mambo katika msingi kwamba endapo vyombo vya
ulinzi na usalama visingebaini mipango hiyo, maana yake ni kwamba tukio ambalo
lingetokea moja kwa moja lingeihusisha serikali ambayo nayo imekuwa ikinyooshewa
vidole, ikidaiwa kuhusika na matukio ya utekaji na utesaji wa watu maarufu kama
ilivyotokea kwa kiongozi wa Jumuiya ya Madaktari nchini, Dk. Steven
Ulimboka.
Taarifa
za kikachero zilizokusanywa na MTANZANIA Jumatano, zimeeleza kuwa ingawa hadi
sasa utekelezaji wa mpango wa kumteka na kumtesa Dk. Ulimboka, uliratibiwa
kiufundi na watu wenye taaluma ya kikachero, walitumia mwanya wa mgomo wa
madaktari kukoleza chuki ya wananchi dhidi ya serikali na kwamba hata
waliofichua uhusika wa mmoja wa maofisa wa Ikulu katika sakata hilo walikuwa na
malengo hayo hayo.
Kwa
upande mwingine, wafuatiliaji wa siasa za mataifa mbalimbali wanasema tukio la
vyama vya upinzani, hususani Chadema kuhusishwa na matukio ya kigaidi huenda
ikawa chama hicho, katika kuhakikisha kinaingia Ikulu, kimeamua kutumia siasa za
staili ya watu wa aina ya Apollo Militon Obote wa Uganda.
Obote,
rais wa zamani wa Uganda, wakati fulani alipoondolewa madarakani chama chake
kilishutumiwa kufanya vitendo vya kigaidi dhidi ya wananchi ili kuwafanya
wajenge taswira mbaya dhidi ya serikali yao.
Vivyo
hivyo inaelezwa kuwa wakati wa utawala wa Iddi Amin nchini Uganda, ambao ulikuwa
ukishutumiwa kwa vitendo vya kinyama, si vyote vilikuwa vikifanywa na serikali
yake, bali inadaiwa kuwa makundi ya misituni yaliyokuwa yakipigana kuingia
madarakani kama yale ya akina Yoweri Museveni, nayo yalishiriki katika vitendo
hivyo, lakini wao hawakuonekana.
Ni kwa
namna hiyo hiyo, matukio ya mauaji ya mwandishi wa habari wa kituo cha Channel
Ten, Daudi Mwangosi na hata kuvamiwa kwa Ofisi za Gazeti la Mwanahalisi na
kujeruhiwa kwa wahariri wake wawili kunaelezwa kuwa unaweza kuwa mpango mahususi
wa kundi la wanausalama lililoasi huku likiwa ndani ya serikali kuichafua
Ikulu.
Tukio
jingine ambalo linaangaliwa kwa mtizamo huo ni kutekwa na kuteswa vibaya kwa
Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri, Absalom Kibanda, anayeaminika kuwa na nguvu ya
ushawishi miongoni mwa wanahabari ambaye aina ya kuteswa kwake inafanana kwa
kiwango kikubwa na ile ya Dk. Ulimboka.
Katika
mwendelezo huo huo wa matukio ya aina hiyo, kuuawa kwa viongozi wa dini, mgogoro
wa kidini wa kuchinja nyama na hata uchomaji moto nyumba za ibada ni vitendo
vinavyodaiwa kutekelezwa makusudi na kundi hilo, lengo likiwa kuamsha hasira za
wananchi dhidi ya serikali.
Hata
hivyo, ni Chadema ambacho sasa kinaonekana kuwa katika wakati mgumu zaidi wa
kujinasua na doa la kuhusishwa na vitendo vya utekaji na utesaji raia kutokana
na mfululizo wa tuhuma za aina hiyo ambazo kimekuwa
kikielekezewa.
Madai
haya yanapewa nguvu na malalamiko yaliyopata kutolewa na Naibu Katibu Mkuu wake,
Zitto Kabwe, ambaye mwishoni mwa mwaka jana akiwa katika mkutano wa kawaida wa
viongozi wa chama hicho, alishutumiwa vikali na viongozi wenzake kwa kukivuruga
Chadema na katika kile kinachoonekana kuumizwa na tuhuma hizo, Zitto alifunua
siri ya mpango wa kumuua aliodai kuandaliwa na viongozi
wenzake.
Sambamba na madai haya ya Zitto, jambo
jingine ambalo limekuwa likikitesa Chadema ni tuhuma za kupanga mauaji ya
aliyekuwa Mbunge wa Tarime, Chacha Wangwe, ambaye harakati zake za kisiasa ndani
ya chama hicho na hasa nia yake ya kuwania uenyekiti ilielezwa kuwa moja ya
sababu za kutekelezwa kwa mauaji
yake.http://www.mtanzania.co.tz
Post a Comment