Rais Kikwete akiwa eneo la tukio tena leo, baada ya kutembelea jana,
akitoa maagizo kwa Kamanda wa Kanda maalumu ya Dar es salaam Suleiman
Kova kwamba kila aliyehusika na ujenzi wa jengo hilo kuanzia mchoraji,
msimamizi na mjenzi wahojiwe na wawajibishwe wakipatikana na kosa
Rais Kikwete akiongea na viongozi wa msikiti wa Shia ithnaasheri wakati anaondoka eneo la tukio
Mkuu wa Polisi Kanda Maalum Mkoa wa Dar es salaam Kamanda Suleiman Kova akifafanua jambo kwa waandishi wa habari katika eneo la Tukio kwenye jengo lililoanguka jana maeneo ya Posta jijini Dar es salaam na kusababisha vifo vya watu, Majeruhi na Uharibifu wa mali, Mpaka mchana huu imethibitika ni watu 20 wamenasuliwa kutoka katika kifusi cha jengo hilo na majeruhi kadhaa, kazi ya uutafuta miili ya watu waliopoteza maisha inaendelea mpaka sasa katika eneo hilo huku vikosi vya ulinzi na usalama pamoja na taasisi mbalimbali vinashirikiana kwa pamoja kuhakikisha vinakamilisha kazi ya kutafuta miili ya watu waliopoteza maisha katika trukio hilo.
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF Profesa Ibrahim Lipumba akihojiwa na mwandishi wa habari wa TBC Grace Kingalame wakati alipotembelea eneo la tukio na kujionea hali halisi ya uokoaji.
Kazi ya kukata nondo ili kuondoa kifusi hicho ikiendelea
Mashine za kuondoa kifusi zikiwa zinaendelea na zoezi hilo.
Post a Comment