RWANDA imeipongeza Tanzania kutokana na mapokezi mazuri ya maafisa wake wa ngazi za juu wa jeshi la nchi hiyo ambao wamefanya ziara ya mafunzo ya siku tano kuanzia Marc 24 hadi 29 mwaka huu ,katika Chuo cha maafisa wa kijeshi kilichopo TMA, Monduli,
Pongezi hizo zimetolewa mjini Arusha, na Balozi mdogo wa Rwanda, Frank Kayijuka, alipokuwa akizungumza na vyombo vya habri kuelezea ziara ya Maafisa wa ngazi za juu wa jeshi la Rwanda, waliofanya ziara ya mafunzo hapa nchini .
Amesema maafisa hao wanatoka katika Chuo cha uongozi wa Kijeshi cha Chuo kipya cha Nyakinama ,kilichopo nchini Rwanda na ni chuo cha kwanza kufanya ziara hiyo hapa nchini
Amesema kuwa katika hstoria ya Rwanda ,hawa ni maafisa wa kwanza kufanya ziara ya mafunzo katka Chuo cha maafisa wa kijeshi hapa nchini ,ambapo kabla ya kusainiwa Itifak ya nchi za jumuia ya afrika mashariki maafisa hao walikuwa wakienda katika mataifa ya Nigeria, uganda, Ghana .
Amesema kuwa hivi sasa wanaona umuhimu wa sana wa kufanya mafunzo hapa Tanania kutokana na kusainiwa kwa Itifaki ya nchi za Afrika mashariki, EAC, kuhusu maswala ya kijeshi ili kubadilishana uzoefu kwa nchi wanachama wa jumuia ya frika mashariki.
Amesema maafisa hao wa ngazi za juu wapatao 28 wenye vyeo kuanzia Meja, na kanali ,wanaongozwa na Brigedia general , Jean Jacques Mupenzi, wamefanya ziara hiyo katika chuo cha maafisa wa kijeshi cha TMA, Monduli

Rwanda imefurahishwa na kuridhishwa sana na mapokezi waliyopata maafisa wake katika Chuo cha maafisa wa Kijeshi cha TMA, Monduli,
Ameongeza kuwa katika itifaki ya jumuia ya afrika mashariki, nchi hizo zinabadilishana maafisa ambao huenda kujifunza maswala ya kijeshi katika nchi wanachama lengo ni kuimarisha mahusiano .
Ameongeza kuwa katika itifaki ya jumuia ya afrika mashariki, nchi hizo zinabadilishana maafisa ambao huenda kujifunza maswala ya kijeshi katika nchi wanachama lengo ni kuimarisha mahusiano .
Amesema kuwa Kauli mbiu ya mafunzo hayo ni maendelo ya Usalama ni nguzo ya taifa
.Amesema kuwa kabla ya kuwasili TMA, Monduli, maafisa hao walifanya ziara nyingine ya siku mbili ya mafunzo makao makuu ya Jeshi jijini Dar es Salaam na wamemalizia ziara yao TMA monduli ambayo ilikuwa ni ya siku tatu ambayo inamalizika March 29 mwaka huu.
Ameongeza kuwa mingoni mwa maafisa hao walishashiriki zoezi la nchi za afrika mashariki lililoitwa Oporation Mlima Kilimanjaro ,lililofanyika hapa nchini mapema mwaka 2009
Amesema maafisa wengine wameenda nchini Uganda kwa mafunzo kama hayo.

Post a Comment