Boniface
Wambura.
Ofisa Habari Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
HONGERA AZAM KWA USHINDI
LIBERIA
Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF) linaipongeza klabu ya Azam kwa ushindi wa mabao 2-1
ilioupata timu yake katika mechi ya raundi ya kwanza ya michuano ya Kombe la
Shirikisho.
Mechi hiyo dhidi ya Barrack
Young Controllers II ilichezwa jana jijini Monrovia, na timu hizo zitarudiana
wikiendi ya Aprili 6 au 7 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es
Salaam.
Ushindi huo unaiweka Azam
chini ya kocha wake Stewart John Hall katika mazingira mazuri ya kusonga mbele
baada ya mechi ya marudiano. Bila shaka ushindi wa timu ya Azam pamoja na mambo
mengine umechangiwa na klabu hiyo kujipanga vizuri.
Hata hivyo ushindi huo bado
ni changamoto kwa wachezaji, benchi la ufundi na uongozi wa Azam kuhakikisha
unajipanga vizuri kwa mechi ya marudiano kwa vile mpira wa miguu una matokeo ya
aina tatu; kushinda, kutoka sare au kufungwa.
Msafara wa timu ya Azam
unaoongozwa na mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, Blassy Kiondo unatarajiwa
kurejea nchini kesho alfajiri kwa ndege ya Kenya Airways kupitia
Nairobi.
TAIFA STARS TRAINING
PROGRAMME
Taifa Stars itacheza mechi
ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia mwaka nchini
Brazil dhidi ya Morocco. Mechi hiyo itachezwa Jumapili katika Uwanja wa Taifa,
Dar es Salaam.
Jumamosi, Machi 16-
Wachezaji kuanza kuripoti kambini
Jumapili, Machi 17- Mazoezi
Uwanja wa Karume- Saa 2 asubuhi
Jumatatu, Machi 18- Mazoezi
Uwanja wa Karume- Saa 9 alasiri
Jumanne, Machi 19- Mazoezi
Uwanja wa Taifa- Saa 9 alasiri
Jumatano, Machi 20- Mazoezi
Uwanja wa Taifa- Saa 2 asub na saa 9 alasiri
Alhamisi, Machi 21- Mazoezi
Uwanja wa Taifa- Saa 9 alasiri
Ijumaa, Machi 22- Mazoezi
Uwanja wa Taifa- Saa 9 alasiri
Jumamosi, Machi 23- Mazoezi
Uwanja wa Taifa- Saa 10.30 jioni
PONGEZI KWA UONGOZI MPYA
TAFCA
Shirikisho la Mpira wa
Miguu Tanzania (TFF) linatoa pongezi kwa uongozi mpya wa Chama cha Makocha wa
Mpira wa Miguu Tanzania (TAFCA) uliochaguliwa katika uchaguzi uliofanyika juzi
(Machi 16 mwaka huu) mjini Dodoma.
Ushindi waliopata viongozi
waliochaguliwa kuongoza chama hicho unaonesha jinsi wajumbe wa Mkutano Mkuu wa
TAFCA walivyo na imani kubwa kwao katika kusimamia taaluma ya ukocha
nchini.
TFF inaahidi kuendeleza
ushirikiano wake kwa Kamati ya Utendaji ya TAFCA chini ya uenyekiti wa Oscar Don
Koroso aliyeibuka mshindi kwa kura zote za ndiyo baada ya kukosa
mpinzani.
Uongozi huo mpya una
changamoto nyingi, kubwa ikiwa ni kuhakikisha unaendesha shughuli za mpira wa
miguu kwa kuzingatia katiba ya TAFCA pamoja na vyombo vya mpira wa miguu vilivyo
juu yake.
Pia tunatoa pongezi kwa
Kamati ya Uchaguzi ya TAFCA chini ya Ramadhan Mambosasa na Kamati ya Uchaguzi ya
TFF kwa kuhakikisha uchaguzi huo unaendeshwa kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi za
Wanachama wa TFF.
Safu nzima ya uongozi wa
TAFCA iliyochaguliwa inaundwa na Dk. Oscar Dan Koroso (Mwenyekiti), Lister
Manyara (Makamu Mwenyekiti), Michael Bundala (Katibu Mkuu), Gabriel Gunda
(Katibu Msaidizi), Dismas Haonga (Mhazini), Wilfred Kidao (mjumbe wa Mkutano
Mkuu wa TFF).
Wajumbe wa Kamati ya
Utendaji waliochaguliwa ni Jemedari Saidi, George Komba na Magoma
Rugora.
Post a Comment