Washindi wa kipindi cha kwanza cha
Guinness Football Challenge kilichooneshwa jana katika Televisheni za ITV na
Clouds TV Mwalimu Akida Hamad(kushoto) na Daniel Msekwa(kulia) katika picha ya
pamoja na waenesha kipindi Flora Tumsiime na Larry Asego jana baada ya
kipindi.
Timu zilizoshiriki kipindi cha
kwanza cha Guinness Football Challenge kutoka kushoto wenye nyekundu ni timu
kutoka Kenya Stephen Githinji na Michael Kirwa, wenye bluu ni Mwalimu Akida na
Daniel Msekwa timu kutoka Tanzania, wenye rangi ya kijani ni timu kutoka Uganda
Kennedy Andindu na Oscar Boban na mwsho timu nyeusi pia ni kutoka Kenya Oscar
Litonde na Daniel Muthendu.
-
Jana usiku kupitia
televisheni za ITV na Clouds TV za jijini Dar Es Salaam,kwa staili
ya GUINNESS® FOOTBALL CHALLENGE™, Daniel Msekwa na Mwalimu Akida
Hamad kutoka Tanzania walioonesha kwamba hakuna kisichoshindikana
na hakuna kufa moyo kabisa katika mchezo huu ambao sasa hivi unatazamwa na wengi
barani Afrika.
Wawili
hao waliishia kwenye sare kwa raundi mbili na kuthubutu kuingia kwenye nusu
fainali ambapo wana nafasi ya kupandisha kitita chao hadi dola za
kimarekani 5,500 (USD 5500) kwenye ukuta wa pesa wa
Guinness.
Daniel
na Mwalimu walionesha umuhimu wa kutokata tamaa na sasa wameingia kwa kishindo
kikubwa kuwakilisha Tanzania kupambana na nchi zingine za Afrika.
Kwenye raundi hii ya kucheza na nchi zingine zilizokuwa kwenye jumuiya ya
Afrika mashariki, ikumbukwe kuwa kuna dola za kimarekani 250,000
($250,000) za kushindaniwa .
Wiki
ijayo tutaweza kuona timu zingine nne kutoka hapa hapa Afrika mashariki
zikichuana vikali na kuonesha umahiri wao, Je wataweza kuingia na kuwakilisha
nchi zao kupambana na nchi zingine za Afrika? Je
timu nyingine kutoka Tanzania itaweza kuwapiga chini wakenya na waganda ili tuwe
na timu mbili kwenye raundi ya ‘Pan Africa ’?
GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE, ni kipindi cha runinga
kinachotayarishwa na kampuni ya kimataifa ya Endemol.
Kipindi hiki kuanzia jana kitakua kinarushwa kila Jumatano katika
televisheni za ITV na clouds TV, kwa ITV itakua ni saa tatu na dakika kumi na
tano(3:15) usiku na saa mbili na dakika kumi na tano(2:15) usiku
Clouds TV.
Usisahau kuwa na chupa ya bia
uipendayo ya Guinness wakati ukitazama kipindi hiki.
*Haiuzwi kwa walio na Umri chini ya miaka kumi
na nane. Tafadhali Kunywa
kistarabu.
Post a Comment