. Airtel, Samsung wakubaliana kukuza soka la vijana
• Airtel Rising Stars Awamu ya tatu kuanza mwishoni mwa mwezi huu
Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel
inayofanyakazi pamoja na kampuni ya Samsung zimesaini makubaliano ya
kushirikiana kudhamini mashindano makubwa Afrika kwa vijana wa chini
ya miaka 17.
Katika mkataba huo wa mamilioni ya dola, Samsung pia itakuwa mtoaji
rasmi wa vifaa vya mawasiliano kwenye mpango huo wa mashindano maarufu
kama Airtel Raising Star (ARS) unaoendeshwa na Airtel.
Airtel inatoa huduma za mawasiliano kwa simu za mkononi kwenye nchi 20
barani Asia na Africa huku Samsung ikiwa ni miongoni mwa makampuni
makubwa ya vifaa vya kisasa vya elektoniki.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jijini Dar es Salaam jana, Airtel
imefanya kazi kwa karibu sana na taasisi za elimu kwenye nchi 17
zinazozungumza Kiingereza na Kifaransa ambapo kwa kupitia mashindano
hayo ya soka ya Airtel Rising Stars yamefanikiwa kushirikisha zaidi ya
timu 18,000.ambapo vijana wa kike na wa kiume wapatao 400,000 barani
Afrika walishiriki katika mashindano hayo ya Airtel Rising Star.

Mwaka jana mashindanoa haya ya Airtel Rising Stars yalionekana kukua
kwa asiliamia 65 na kuna kila dalili kwa mwaka huu kukua zaidi,”
inasomeka sehemu ya taarifa hiyo iliyotolewa na Airtel Makao Makuu.
Mkakati huo wa kukuza soka barani Afrika unaungwa mkono kwa dhati na
klabu kubwa za England; Arsenal FC na Manchester United ukiwa na lengo
la kuibua na kukuza vipaji vipya vya vijana wa Kiafrika.
“ARS imefikia kuwa chanzo kizuri cha wachezaji wapya wa timu za
mataifa mbalimbali huku pia wengine wakijiunga na klabu zinazoshiriki
ligi kuu barani humu. Afrika ina vijana wengi zaidi duniani. Uwiano wa
vijana barani humu ni mkubwa kuliko mabara yote kwani takwimu
zinaonyesha kuwa asilimia 60 ya Waafrika zaidi ya bilioni moja ni
vijana,” alisema George Ferreira, Makamu wa Rais wa Samsung
Electronics, Africa.
Akizungumzia ushirikiano huo, Andre Beyers, Ofisa Masoko Mkuu wa
Airtel Africa alisema: “Ushirikiano huu utapanua wigo wa biashara na
kuyawezesha mashindano ya ARS kufikia malengo yake.”
Msimu ujao wa Airtel Rising Stars ukiwa ni wa tatu tangu kuanzishwa
kwake utaanza mwishoni mwa mwezi huu.
Moja kati ya matunda ya mashindano haya ya Airtel ni Priscilla Okyere,
binti aliyeibuka kutoka ARS na sasa ni nahodha wa timu ya taifa ya
wasichana chini ya miaka 17 ya Ghana. Aliiongoza timu hiyo kunyakua
medali ya fedha kwenye mashindano ya Dunia ya FIFA Under-17 kwa
wanawake mwaka jana huko Azerbaijan.
Post a Comment