Mara baada ya matokeo ya kidato cha nne 2012 kutoka nilifungua uwanja kwa wadau kutafuta chanzo cha tatizo kupitia kuuliza swali na wao walijibu.
Asilimia 37 sawa na kura 90 kati ya 244 walisema MITAALA YA KUFUNDISHIA ni tatizo la kushuka kwa kiwango cha elimu nchini.
Halikadhalika asilimia 35 sawa na kura 86 walisema WANAFUNZI WENYEWE ndio tatizo la kushuka kwa kiwango cha elimu nchini.
Asilimia 18 sawa na kura 45 walisema WAALIMU ni tatizo cha kushuka kwa kiwango cha elimu nchini. Na matokeo mengine ni kama yanavyoonekana.
Na haya yafuatayo ni baadhi ya maoni ya wadau kama walivyoyatoa :
Nora Diaby on March 19, 2013 at 5:40 am.
Waalimu wenyewe wamewaangusha watoto wetu.
Posted by maseka on March 5, 2013 at 12:24 pm. From 196.43.67.x Report Abuse
mitaala inabadilishwa sana na walimu wengi shuleni hawapati mabadiliko hayo mapema hivyo huendelea na mitaala ileile ya zamani kwani hiyo mipya huwa hawaijui na hawajapewa semina jinsi ya kuitumia na walimu wachache hupata nafasi ya semina hiyo
Posted by MHANGA on March 4, 2013 at 4:53 am. From 41.204.151.x Report Abuse
wanafunzi wengi hawajitambui na hawatambui nn wanakihitaji huko kwenye vituo vya elimu
Posted by ally on March 3, 2013 at 2:01 am. From 197.152.57.x Report Abuse
wanafuzi starehe sana
Posted by Nyamilele on February 26, 2013 at 10:20 am. From 41.59.17.x Report Abuse
mitaala iliyoanzishwa bado haijazoeleka kwa wanafunzi kuweza kujibia maswali ya mitihan nashauri ingeanzia darasa la tano hadi kufika sekondali wanafunzi wanakuwa wamezoea. hivyo itakuwa rahisi kujibu maswali
N.B Maoni haya si msimamo wa mmiliki wa blog hii bali ni maoni ya wasomaji wa blog ya NDGSHILATU
N.B Maoni haya si msimamo wa mmiliki wa blog hii bali ni maoni ya wasomaji wa blog ya NDGSHILATU
Post a Comment