Inaelezwa kwamba iwapo Afrika inataka kukomesha
njaa lazima iandae mpango rahisi kwa wakulima milioni 900 ambapo kuna uwezekano
wa kuongezeka kwa mapato ya wakulima kwa asilimia 80.
Jambo hilo linafanya gharama za
uzalishaji zinatakiwa ziwe zimepunguzwa kwa kiwango kikubwa sana
"Tizameni kule" anatamka
hayo Vincent Ssoko akimaanisha kule kwenye majani ya kijani ya migomba ambayo
haitamaniki .ikiyumba kutokana na kipepo cha joto ikiwa imezungukwa na
senyen'ge.Anasema "Daima nimekuwa nikiwambia jirani yangu kwamba fanya
kama nilivyofanya mimi.Chimba shimo kubwa ili kuufanya mti huo uwe na nafasi ya
kutosha,jaza mbolea ya kutosha na uhakishe kwamba mbegu hazipandwi kwa
kukaribiana."Jirani huyo anananuwa tena mbolea ya ghali na kufidia mavuno
mabaya.
Vincent Ssoko mkulima wa
bio(anayetumia ukulima wa asili bila ya kemikali) huko Busana katika mkoa wa
Kayunga ambapo huchukuwa kama saa tatu kwa mwendo wa gari kutoka kaskazini
mashariki mwa mji mkuu wa Uganda, Kampala ana sababu nzuri ya kutabasamu.Kwani
alikuwa ndio kwanza amenenuwa tena hekta 20 za ardhi ziada ya hekta 29
alizokuwa nazo. Anasema hapo mwaka 1998 alianza na hekta tatu. Mkulima huyo
mwenye umri wa miaka 46 hivi sasa anaotesha mananasi, ndizi, kahawa na maharage
kwa njia ya bio... na hasa kwa kuwa na cheti cha bio.Kwa hiyo anaweza
kusafirisha mazao yake hayo katika soko la bara la Ulaya. Anaonyesha kwa fahari
manasi matamu yalioteshwa kwenye mstari mrefu ulionyooka.Zaidi ya nusu ya
matunda 700,000 kwa mwaka yanakwenda Ujerumani.Ssoko hujipatia shilingi 700 za
Uganda sawa na senti 20 za euro kwa tunda moja.Katika soko la ndani ya nchi
huwa anajipatia tu shilingi 150 tu sawa na centi nne za euro.
Iwapo Afrika inataka kukomesha njaa
lazima iandae mpango rahisi kwa wakulima milioni 900: Ni dhahiri kwamba mapato lazima
yaongezwe na wakati huo huo gharama za uzalishaji hazina budi kupunguzwa kwa
kiwango kikubwa sana.Uchunguzi kabambe uliofanywa na Shirika la Mpango wa
Mazingira la Umoja wa Mataifa (UNEP) hapo mwaka 2010 umedokeza kwamba mambo
yanakwenda vizuri : Uchunguzi miongoni mwa mashamba milioni kumi na mbili
takriban katika nchi 60 zinazoendelea umebaini kwamba wastani wa mapato
huongezeka kwa hadi asilimia themanini wakati konde zinapolimwa kwa misingi ya
ekolojia.Uganda ilioko Afrika Mashariki ni aina ya maabara ya majaribio.Vincent
Ssoko anasema badala ya kununuwa madawa yalio ghali anatumia mbolea ya asili
anayoipata bure kutokana na wanyama wake na kwamba badala ya kutumia madawa ya
kuulia wadudu anatumia mkojo na majivu kupambana na wadudu hao waharibifu wa
mazao.Kwa kazi ya kun'gowa magugu pekee mkulima huyo inabidi amlipe mtu,kwani
hapa pia ni marufuku kutumia madawa ya kuuwa magugu.
Bio kwa watu wote
Katika mji mkuu wa Kampala Judith
Nabatanzi akiwa mwenye motisha anapiga chapa kwa kutumia kompyuta yake.Judith
na mwenzake Cathy Kyazike wanaongoza kwa pamoja '' Duka la Mazao ya Kilimo
Asilia '' - au "Nunua Mazao ya Kilimo Asilia ''.Ni jina la mradi wa duka
hilo dogo ambalo lina mazao ya matunda na mboga mboga za aina mbali mbali
yaliyozalishwa kwa utaratibu wa kilimo asilia kuanzia vikonyo vya vanila hadi
karoti.Duka hilo linamilikiwa na Nogamu shirika mama la wakulima wanaofuta
utaratibu wa kilimo asilia nchini Uganda na ni duka pekee la matunda na mboga
mboga za bio zenye kuzalishwa kwa utaratibu wa asili nchini Uganda nchi yenye
idadi ya watu miloini 35.
Kuanzia saa moja asubuhi Judith
tayari anakuwa dukani kushughulkia oda za wateja wake.Anasema Ijumaa ni ndio
siku kuu ya biashara katika kipindi cha wiki kutokana na kwamba wengi wa wateja
wao wanataka kupika mwishoni mwa juma. Kwa hiyo inabidi wafunge vikapu vya
mahitaji ya wateja takriban arobaini au hata zaidi,wakati huo wakulima
waliowasili mwanzo wakiwa wameegesha kwenye mlango wa duka hilo na Boda Boda
yaani taxi za pikipiki kama zinavyojulikana nchini Uganda.Siku moja kabla
wakulima huwa wanazungumza kwa njia ya simu na Judith na Cathy kuwapa bei za
mazao yao, asubuhi inayofuata wakulima huleta mazao yao dukani kwa kuondoka
kutoka maeneo ya ndani mashambani na mapema kuepuka msongamano wa magari.
Shamba la Ssozi Muwangwa liko kama
kilomita 30 magharibi kutoka Kampala. Mkulima huyu huyapakia maboksi yake ya
nyanya kwenye pikipiki na anakwenda kwenye duka hilo mara moja kila wiki tokea
mwaka 2007.Anaona bei za hapo ni nzuri kuliko bei za mazao ya kawaida yaani
shilingi elfu nne sawa na euro moja centi kumi na tano kwa kilo ambayo ni bei
nzuri zaidi kuliko ile ilioko kwenye soko la barabarani.Je inamaanisha kwamba
anaweza kuthibitisha utafiti wa shirika la Mpango wa Mazingira la Umoja wa
Mataifa UNEP kwamba mapato yanayotokana na mazao ya bio ni ya juu? Akiunga
mkono uchunguzi huo wa UNEP Muwangwa anasema inakuwa ni kawaida kwa ardhi kuwa
na rutuba bila ya kutumiwa kwa madawa ya kemikali na wanazalisha kwa wingi tena
kwa kipindi kirefu pamoja na kuepuka ughali wa mbolea. Kwa jumla hujipatia
mapato makubwa ya asilimia 30 na mara nyengine hata hamsini.
Wakati Muwangwa anapopakuwa maboxi
yake Judia na Cathy huchambuwa oda zao na kutumbukiza kwenye vikapu matunda na
mboga mboga mbali mbali kuanzia saladi, matufaa na karoti.Juu ya vikapu hivyo
huwekwa karatasi za oda ili kuepusha mparaganyiko. Mbali ya Boda Boda pia
kunakuwepo na magari yenye vipoza joto kwa ajili ya kuchukuwa vitu vinavyoweza
kuharibika haraka vinaposafirishwa wakati wa asubuhi kutokana na joto lenye
unyevu.
Wakulima wachache wa bio wana avyeti
Moses Muwanga anasema utaratibu wa
kupata cheti cha bio kwa wakulima una gharama kubwa sana.Anakiri kwamba
amesaidiwa na Nogamu chama cha wakulima wa Bio wenye kutumia kilimo asilia
kugharamia cheti chake lakini wakulima wengi bado wanashindwa kuvilipia vyeti
hivyo .Bei ya cheti hicho ni dola 24,000.(Muwanga anakunywa fundo moja la chai
yake yenye cheti cha bio wakati akitafakari mahesabu hayo.)Muwanga ambaye ni
kiongozi wa Nogamu kwenye ukuta wa ofisi yake kumetundikwa vyeti vya wteja wake
kutoka Japani,Marekani na Umoja wa Ulaya ambao wote hao hao wametowa leseni kwa
bidhaa za chama cha wakulima wa Bio nchini Uganda ,Nogamu.Kwa mujibu wa Muwanga
ziara za wakaguzi hugharimu dola elfu nane.Zinahitajika elfu kumi na sita
kubadili uoteshaji wa mazao wa kawaida na kuingia kwenye ule wa bio wa kutumia
kilimo cha asili yaani bila ya matumizi ya madawa ya kemikali,hatua ambayo
huchukuwa mwaka mzima. Kwa hivi sasa Nogamu inafanya kazi na wakulima wadogo wa
bio milioni mbili lakini ni laki mbili tu ndio wenye vyeti ya kimataifa vya
kusafrisha nje mazao yao. a
Siasa lazima ihitaji bio
' Suali hilo pia linamfikia mkuu wa
chama cha wakulima wa bio : Kweli barani Afrika inawezekana kuongeza mapato
hadi asilimia 80 kwa kilimo cha biolojia ? Kwa mujibu wa Muwanga anasema wao
wameorodhesha kesi ambapo mapato ya mkulima yameongezeka maradufu baada ya
kubadili kilimo na kuingia kile cha bio.Ardhi yake haiathiriwi na madawa ya
kemikali na ndio maana kwa haraka inaleta tija lakini siasa haijatambuwa hilo
kwa wakati unaotakiwa anakosoa Muwanga na kuemndelea kuisema kwamba" Bio
manake pia ni uhifadhi hai wa mazingira,utaratibu huo wa kilimo asilia una
vyakula zaidi na lishe ya kutosha, Mapato kwa wananchi yanazidi asilimia 80 na
una nafasi kubwa kusafirishwa nje kwa bidhaa zake." Nchini Uganda
usafirishaji nje wa mazao ya kilimo cha kawaida umekuwa ukipunguwa. Kwa miaka
sita sasa muswada wa sheria juu ya kilimo endelevu cha bio umekuwa ukijadiliwa
miongoni mwa wabunge.Muwanga anatumai pegine hatimae mwaka huu unaweza
kupitishwa.
Wakati Moses Muwanga alipokuwa
Ujerumani mwaka 2012 alitembelea Maonyesho ya Bidhaa za Bio na kupatiwa oda
zenye thamani ya dola miloni mia mbili.Lakini hadi sasa Uganda inaweza tu
kupeleka bidhaa za bio za thamani ya dola milioni 40.
Mwandishi :Ludger Schadomsky/
Mohamed Dahman
Mhariri: Alakonya, Bruce
Post a Comment