Dar es Salaam. Mkurugenzi wa
Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba amerejea jana akitokea nchini
Afrika Kusini alikokuwa akitibiwa kwa zaidi ya miezi miwili.
DCI Manumba alisafirishwa kwenda nchini Afrika Kusini Januari 26, mwaka huu kwa matibabu zaidi baada ya kulazwa katika Chumba cha Wagonjwa Mahututi (ICU) cha Hospitali ya Aga Khan tangu Januari 13, mwaka huu.
DCI Manumba alisafirishwa kwenda nchini Afrika Kusini Januari 26, mwaka huu kwa matibabu zaidi baada ya kulazwa katika Chumba cha Wagonjwa Mahututi (ICU) cha Hospitali ya Aga Khan tangu Januari 13, mwaka huu.
Tangu alipolazwa Aga Khan,akiwa hajitambui huku akipumua kwa msaada wa mashine, viongozi mbalimbali wakiwamo wa Serikali walimtembelea ili kumjulia hali.
Manumba alikuwa amelazwa katika Hospitali Millpark iliyopo Afrika Kusini.
Ilielezwa kuwa Manumba alikutwa na vijidudu 500 vya malaria, idadi ambayo ni kubwa na inaelezwa kusababisha figo kushindwa kufanya kazi, pamoja na kupoteza fahamu.
Taarifa iliyotolewa jana na Msemaji wa Polisi nchini, Advera Senso ilieleza kuwa DCI Manumba,amerejea baada ya madaktari waliokuwa wakimtibu kuona afya yake imeimarika kiasi cha kuridhisha.
“Amerejea majira ya saa 7:00 mchana, polisi inawashukuru wananchi wote waliokuwa wakimuombea,” alisema Senso katika taarifa yake.
Hivi karibuni akiwa Afrika Kusini, Manumba alisema ugonjwa wake ulimfanya ashindwe kujitambua kwa siku 42 na atakapopona atarejea nchini kuendelea na kazi yake kama kawaida.
Manumba ambaye alilazwa nchini Afrika Kusini alikuwa akifanya mazoezi mepesi ya kusimama na kutembea kama sehemu ya matibabu
yake.
“Ninawashukuru madaktari, wamejitahidi maana ni kama watu walishakata tamaa kwamba siwezi kupona,” alisema Manumba alipozungumza na gazeti hili alipolazwa hospitali hiyo iliyokoe mjini Johannesburg.
Manumba alisema ni kwa mkono wa Mungu amepata nafuu kubwa baada ya juhudi kubwa za madakari katika kupigania uhai wake na kuwashukuru madakari wapatao watano, kila mmoja akijishughulisha na eneo lake kwani ndiyo waliookoa maisha yake.
Mwananchi
Post a Comment