Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

FREEMAN MBOWE AMKAANGA ZITO KABWE

* ADAI KUWA LWAKATARE HATOFUKUZWA CHADEMA HATA KAMA NI GAIDI


                                                     **********

Katika hali ya kushitua,Mh.Mbowe akiongea na wanachama wa chadema leo Ubungo plaza amemkaanga Zitto kabwe na kudai kuwa chadema haiko tayari kumtimua Lwakatare katika chama hata kama ni gaidi....

"Eti nashangaa kuna watu wanataka CHADEMA kimuache Lwakatare na kumsimamisha uongozi kwa uzushi uliopandikizwa na CCM, Hilo halitafanyika"- alisema Mbowe.

IKUMBUKWE siku chache zilizopita naibu katibu Mkuu wa
CHADEMA Mh. Zitto Kabwe alitoa mapendekezo ya kuomba Mshitakiwa mkuu kwenye kesi ya Ugaidi ambaye ni Ndugu Lwakatare aliyekuwa mkuu wa usalama wa chadema awajibike kisiasa...

Kuwajibika kisiasa ni pamoja na kuachia ngazi ya ukurugenzi wa usalama ili kupisha uchunguzi salama na kukiacha chama salama.

Katika barua yake kwa chama chake,Zitto Kabwe alikitaka chama kijichunguze kuhusu shutuma hizi za ugaidi zinazokikabili huku Lwakatare akiwa nje ya ulingo wa viongozi waandamizi wa chadema.

Hata hivyo katika hali ya kustaabisha barua ya zitto ilivuja na kusambaa mitandaoni wakati Zitto Kabwe anadai kuwa ilikuwa ni barua ya siri kati yake na ofisi ya katibu mkuu wa chadema....

Kauli ya Mbowe leo hii kumkana zitto Kabwe mbele ya wanachama wa inaleta sura mbili ndani ya chama hicho cha upinzani:

Mosi:Barua ya mapendekezo ya Zitto ilivujishwa kwa maksudi kama njia ya kumpinga zitto....

Pili: Kauli ya Mbowe ya leo inamkingia kifua katibu mkuu kutowajibika kwa kuvujisha barua kwa sababu barua haikubeba ujumbe wenye maana kwa chama na Lwakatare

Tatu: Madai ya UGAIDI dhidi ya Lwakatare na Chadema kwa ujumla ni ya kweli ,hivyo chama kinajukumu la kumlinda Lwakatare ili kuuficha ukweli usijulikane
 
MASHIHO 150 BLOG
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top