Mbunge Wa Arusha Mjini Godbless Lema akiwa katika chuo cha Uhasibu, Arusha kabla ya kuzuka kwa vurugu hapo jana.
MKUU wa Mkoa wa Arusha,
Magesa Mulongo ameamuru polisi kumkamata Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema
pamoja na wanafunzi walioshiriki kurusha mawe baada ya kutokea vurugu
zilizotokana na kifo cha mwanafunzi wa mwaka wa pili, Chuo cha Uhasibu Arusha,
Henry Kago (22).
Naibu Mkuu wa Chuo cha
Uhasibu Arusha, Faraji Kasidi jana alitangaza kufunga chuo hicho kwa muda
usiojulikana kutokana na vurugu zilizotokea chuoni hapo, ikiwemo ukiukwaji wa
nidhamu na urushwaji wa mawe uliofanywa na wanafunzi hao kwa Mkuu wa Mkoa na
kamati ya ulinzi na usalama.
Mulongo alitoa amri hiyo
baada ya Lema kudaiwa kuingia chuoni hapo jana asubuhi na kufanya siasa bila
kufuata utaratibu.
“Si jambo jema kwa
Mbunge kuingia chuoni na kuhamasisha siasa kwenye jambo hilo la kifo badala ya
kuwatuliza wanafunzi ili tujue kiini cha tatizo hili," alisema mkuu wa mkoa na
kushutumu kwamba jambo hilo linabadilika badala ya msiba linawekwa chuki za
siasa na wanafunzi nao kuingia kwenye mkumbo.
Kwa mujibu wa mkuu wa
mkoa, upo utata wa kifo cha Kago kutokana na wengine kudai ameuliwa na bodaboda
eneo la Esami na Kanisa la Waadventista Wasabato karibu na chuo huku wengine
wakidai alitoka eneo la Bugaluu.
Alisema polisi
inachunguza utata wa kifo hicho cha mwanafunzi huyo aliyekutwa na simu yake ya
mkononi.
"Naagiza
polisi kumkamata Lema popote alipo na wanafunzi wengine pamoja na wakili wake,”
alisema Mkuu wa Mkoa bila kutaja jina la wakili.
Kwa mujibu pia wa RADIO
FIVE ya jijini Arusha, Mkuu huyo wa mkoa wa Arusha bwana Mulongo amenukuliwa
kwa nyakati tofauti tangu jana akitaja uwezekano wa Lema kusababisha kifo cha
mwanafunzi ili apate nafasi ya kufanya siasa chuoni hapo.
Credit: Habarileo na
Radio five
1 comments:
vitu vingine fanyeni uchunguzi kwanza...sababu lema ndie alietuliza vurugu, na sivyo anavyosema huyo mkuu wa mkoa, sababu kutokana na yeye ndie aliesababisha vurugu...na yeye ndie alionesha chuki kwa lema na kuwadharau wanafunzi ,,haiwezekani watu wenye akili zao , waanzishe mnazoziita vurugu pasi na sababu ya msingi...WAHOJIWE WANAFUNZI WALIOKUEPO KWENYE HIZO VURUGU , PIA KULIKUA NA WATU WANAREKODI VIDEO ZIFUATILIWE KUUJUA UKWELI
ReplyPost a Comment