Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

HII NI KWA WALE VIJANA WATAKAOJIUNGA NA MAFUNZO YA JKT

Dhumuni la mkutano huu, ni kutoa ufafanuzi/maelezo ya Mpango mpya wa kujiunga na JKT (Compulsory programme) kwa wanafunzi watakaohitimu Kidato cha Sita 2013. Mpango ambao uliwahi kuwepo hapo awali. Pia utawahakikishia fursa ya kufafanuliwa maswali na dukuduku zenu.Ikumbukwe kwamba Vijana wamekuwa wakishirikiswa katika suala la ulinzi wa Jamii zao tangu enzi za kabla ya Uhuru. Kwa mfano Wayao(Ndagala), Wamakua(Mmera), Wagogo(Ikumbi), Wanyaturu(Misanga), Wamasai(Manyata) n.kMafunzo hayo katika makabila mbalimbali yalikuwa yakitolewa wakati wa mafunzo ya Jando na UnyagoMafunzo yaliyotolewa katika makambi hayo yalihusu ukakamavu, uhodari katika kufanya kazi za kilimo na ufugaji, ulinzi , nidhamu, ushujaa na adabu njema na malezi ya familia.Nchi mbalimbali pia zimekuwa na program za kuwaandaa vijana wake. Kwa mfano Zambia ( National Service), Kenya ( National Youth Service), Ghana ( National Service Scheme), China (Poverty Alleviation Relay Project), New Zealand ( Conservation Corps), Nigeria ( National Youth Service), Namibia ( National Youth service), Malaysia ( National Youth Scheme), Israel (National Youth Scheme) n.kNchi mbalimbali ikiwemo Msumbiji, Afrika Kusini, Rwanda zimeshatuma wawakilishi wao kutembelea JKT kujifunza jinsi ya kuanzisha mafunzo kama hayo katika nchi zao.Aidha, Sera ya Ulinzi na Usalama wa nchi yetu inatamka bayana kwamba wajibu wa kuilinda nchi yetu ni ya Mwananchi wenyewe na hasa ninyi Vijana.
 
Ninyi vijana hamtokuwa wa kwanza kupitia katika program hii, kwani Watanzania wengi wakiwemo Viongozi wa Idara za Serikali, Mashirika ya Umma, Wakurugenzi, Viongozi katika Asasi binafsi na hata Viongozi wa Kitaifa ( Mawaziri Wakuu na Ma-Rais) pia walifaidika na mpango huo Wazo la kuanzisha
JKT katika Tanzania lilijadiliwa kwa mara ya kwanza katika mkutano wa mwaka wa Umoja wa Vijana wa TANU ( T.Y.L) uliofanyika mjini Tabora, mwaka 1962.19 Apr 63 Baraza la Mawaziri liliidhinisha kuanzishwa kwa mpango huo baada ya kufanya marekebisho yaliyohitajika.Mnamo tarehe 10 Jul 63 JKT ilianzishwa rasmi kwa kuandikishwa vijana 11 kutoka Wilaya 11. Vijana hao wa mwanzo walikuwa Makatibu wa Umoja wa Vijana katika Wilaya zao.Kukua kwa JKT (1963 – 1994)Vijana wa kujitolea waliendelea kuongezeka kwa ajili ya kupata mafunzo ya uzalendo, ujasiriamali na Uongozi.KUNDI LA AWALI LA VIJANA WALIOJIUNGA NA MAFUNZO YA JKT MWAKA 1963 Uamuzi wa kuwachukua vijana wa Mujibu wa Sheria waliohitimu Kidato cha Sita na vyuo kujiunga na JKT ulifikiwa rasmi mwaka 1965.Mwalimu Nyerere alitoa tamko hilo pale Arnautoglu Hall, ambapo aliwataka vijana wasomi wote nchini kujiunga na JKT.Bunge lilifanya marekebisho ya Sheria mwaka 1966 (Act of Parliament No 64 of 1966) yaliyompa madaraka Mkuu wa JKT kuwaita vijana wa Mujibu wa Sheria. Kutokana na kuongezeka kwa wingi wa vijana wa kujitolea na wale wa mujibu wa sheria, wigo wa shughuli na makambi ya JKT ukapanuka, hivyokulazimika kuanzishwa makambi kama vile Oljoro, Itende, Buhemba, Mpwapwa, Mafinga n.k.Mwaka 1975 yalifanyika marekebisho ya muundo wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania na JKT kuwa miongoni mwa fomesheni (sehemu) ya Jeshi hilo.Fomesheni hii ya JKT ilipewa majukumu ya kuwafundisha vijana kulitumikia Taifa, kwa kushiriki shughuli mbalimbali za Kijamii, Mendeleo, Uchumi na Ulinzi.Fomesheni hii ya JKT ilipewa majukumu ya kuwafundisha vijana kulitumikia Taifa, kwa kushiriki shughuli mbalimbali za Kijamii, Mendeleo, Uchumi na Ulinzi. Pia kutoa mafunzo ya kijeshi kwa vijana kwa lengo la kuwaandaa kujiunga na vyombo vingine vya ulinzi na usalama. Na kwa ujumla kushiriki kikamilifu katika ulinzi wa Taifa na kusaidia kuokoa watu na mali wakati wa majanga ya kitaifa.Kusitishwa kwa JKT (1994)Ilipofika mwaka 1994, Serikali iliamua kusitisha mafunzo ya JKT kwa sababu za kiuchumi, na shinikizo kutoka Benki ya DuniaHadi kufikia mwaka 1994 shughuli za JKT zilikuwa zimepanuka sana kwa maana ya miundombinu yake, rasilimali watu, vifaa vya mafunzo, wanafunzi, n.k.Vijana 262,704 walikuwa wamefaidika na mafunzo ya JKTKurejeshwa Mpango wa Vijana Kujiunga na JKT.Hatua ya kusitisha mafunzo hayo haikupokelewa vema na jamii ya Watanzania hatimaye kuitaka Serikali kutafakari upya uamuzi huo.Hivyo mwaka 2001, Serikali ilirejesha utaratibu wa vijana kujiunga na mafunzo ya JKT kwa kujitoleaChini ya utaratibu huo, vijana wapatao 5,000 wamekuwa wakichukuliwa kila mwaka kwa kujitolea.Hadi sasa vijana takribani 42,661 (wavulana 33,054 na wasichana 9,607) wamefaidika na mafunzo haya.Hata hivyo, Serikali haikuweza kurejesha utaratibu wa kuchukua vijana kwa mujibu wa Sheria kutokana na uhaba wa fedha ,Ingawa imekuwa ikitenga fedha kwa ajili ya maandalizi ya kuwapokea vijana hao makambiniSerikali imeona ni vyema sasa utaratibu wa kuchukua Vijana kwa Mujibu wa Sheria urejeshwe kuanzia mwaka 2013 kwa kundi dogo la vijana kwa kuanzia na vijana 5,000 watakaotoka katika kundi kubwa la vijana watakaohitimu Elimu ya Kidato cha Sita (41,348)Ni dhahiri kundi hilo ni dogo ikilinganishwa na idadi kubwa ya wahitimu. Ni dhahiri pia kwamba vigezo vyovyote vitakavyotumika kupata vijana hawa 5,000 vitaacha changamoto ya haki sawa kwa wote. Hivyo basi, kwa vyovyote vile, ninyi ni miongoni mwa vijana wachache waliopata bahati hiyo ya kuanzisha tena mpango mpya wa mujibu wa sheria katika kundi la kuanzia.Vigezo vilivyotumika kuwapata vijana 5,000Serikali imeona ni vyema Kundi hili la vijana 5000 wa kuanzia wapatikane kutokana na uwakilishi kutoka shule mbalimbali zenye asili tofauti kwa kuzingatia vigezo kama vile: Jinsia, mtawanyiko kitaifa, aina ya shule (serikali, binafsi, n.k), uwezo wa shule kitaaluma, n.k. Baada ya Serikali kuweka vigezo hivyo, shule yenu imebahatika kuwa miongoni mwa shule chache nchini, ambazo zimepata fursa hiyo adhimu .Hongereni sana!Faida za Fursa hiyoZaidi ya vijana kujengewa nidhamu, ukakamavu, fikra za utaifa, kulinda amani, utangamavu, uwezo wa kujitegemea, utaifa, utu na uwezo wa kusimamia rasilimali za Taifa. Pia, utapata faida za ziada kama vile:-

  • Sifa za ziada za upatikanaji wa fursa za ajira Serikalini .
  • Fursa ya kupata stadi za uongozi.
  • Kupanua wigo wa mahusiano miongoni mwao (PR)
  • Kujengewa uwezo wa kuanzisha mradi wako, mara baada ya kupata mafunzo ya ujasiriamali JKT.
  • Mtatunukiwa vyeti, kama kielelezo cha ushiriki wako katika mpango huu adhimu wa Taifa. Matarajio ya JKT na Serikali
Ni matarajio ya Serikali kwamba, mtapokea wito huu kwa dhati na ari kubwa na kwamba mtashiriki kwa uaminifu na uhodari mkubwa.Aidha, kwa upande wetu JKT, tunategemea Ushirikiano wenu katika kuitikia wito huu wa Serikali kwa kuripoti kwa wakati makambini.Pia kwa upande wetu wa JKT, tunaahidi kuwapokea na kutekeleza mafunzo ya JKT kwa weledi mkubwa.Tunaahidi kwa niaba ya Uongozi mzima wa JKT na Wizara kwa ujumla, kwamba mafunzo yataratibiwa kitaalamu bila kuathiri maisha ya wanafunzi.Maandalizi yote ya msingi kwa ajili ya mafunzo yenu yameshakamilika na kinachosubiriwa kwa sasa ni ninyi kuripoti makambini.Haki zenu za msingi kama vile posho, malazi,chakula, matibabu, maji, na burudani n.k.) zitaratibiwa ipasavyo.Lakini pia, tungependa tuwakumbushe kwamba, sheria ya wito wa kujiunga na JKT kwa mujibu wa sheria bado ipo na haijafanyiwa marekebisho, kwa hiyo ni wajibu wa kila anayepaswa kujiunga na mafunzo hayo, kutekeleza jukumu hilo bila kusita.HITIMISHOAsanteni sana kwa Kunisikiliza

Source: http://jkt.go.tz/mada-ya-vijana-wa-mujibu-wa-sheria.h
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top