kulalamikia Vitendo vya watendaji/Wakuu wa Idara kuacha magari na
Vifaa vya Halmashauri hiyo Bila ya Matengenezo ili vichakae na kupanga mipango ya kujiuzia mali za halmashauri hiyo kinyemela bila ya kufuata kanuni na taratibu zilizopo.
Malalamiko hayo yamejitokeza baada ya hoja iliyotolewa na Diwani wa kata ya Kilangala, Haridi Chilumba kutoa hoja ya kutaka maelezo juu mpango mkakati wa halmashauri hiyo kuondoa tatizo la upungufu wa Vyombo vya usafiri na usafirishaji ili kurahisisha Huduma za
Halmashauri hiyo.
Chilumba alisema halmashauri hiyo inakabiliwa na upungufu mkubwa wa magari japo kuwa kuna magari zaidi ya kumi ambayo hayaonekani
yakitembea na kufanya kazi za halmashauri,
Nakumbuka baadhi ya namba za magari kuwa SM 4044 ya Idara ya
Kilimo, SM3008 Elimu DFP 4083 DFP 6992, DFP 3014, STK 1380 SM2904 hazionekani barabarani na sisi madiwani hatupewi taarifa
yoyote?Alihoji Chilumba.
Mweka hazina wa halmashauri hiyo Dk Haule alisema kuwa magari hayo yameharibika na baadhi ya hayo vipuri vyake upatikana nje ya nchi kutokana na muundowake kutokuwepo na kutokuwa na wataalamu waliobobea katika sekta hiyo ndani ya Halmashauri yetu.
Dk Haule alisema kuwa ubovu wa magaria hayo ni mkubwa kwani yapo ambayo hayatengenezeki kabisa na mengine yana matatizo ya gear box, injini na uchakavu wa matairi kwa kiasi kikubwa na kama mnavyojua hali ya Halmashauri yetu,
Kufuatia majibu hayo,Ahmadi Mussa Mbonde Diwani wa kata ya Mtumbya alisema kuwa kitendo cha magari hayo kuwa mabovu bila ya kupewa taarifa madiwani ni njama ya watendaji hao kutaka kujiuzia wenyewe.
Haiwezekani magari yote kumi yakawa mabovu wakati halmashauri
imeajiri mafundi kwa ajili ya kufanya marekebisho ya magari hayo.
“Unajua ipo tabia ya watendaji kujiandalia mpango wa kujiuzia magari
ya halmashauri kinyemela wakati madiwani wakiondoka na kubaki Wao katika kikao cha kamati ya watendaji pekee (CMT) Tabia hii hatuwezi kuicha ikiota mizizi katika halmashauri yetu iliyo masikini
Sasa ni vizuri madiwani tukaunda tume maalumu ya kwenda kuangalia
ubovu wa magari hayo ili kutambua matatizo yake ” Hoja ilitolewa na
Diwani Mbonde.
Kwa upande wake mkurugenzi mtendaji wa halmashauri hiyo, Bi Grace
Mbaruku aliwataka madiwani hao kuwa watulivu na kuiachia kazi hiyo kamati ya fedha utawala na mipango kufuatilia suala hilo na kikao
kijacho itolewe taarifa.
Waheshimiwa Madiwani Mimi ni mgeni katika Halmashauri hii nimeripoti na kukuta kikao hiki kikubwa. Naomba kutoa rai kwenu mniachie suala hili nilifuatilie niyaone na nipate maelezo ya Wakuu wa Idara Husika ikiwa pamoja na kukabidhiwa rasmi mali za Halmashauri
Nitatoa taarifa katika kamati ya Fedha na baadae mtaamua kutokana na hiyo taarifa, Nawaomba waheshimiwa Mimi pia ni Mchumi Nafahamu, Bi Grace aliomba Baraza
Kikao cha Tatu cha Baraza hilo Pia kiliudhuriwa na Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Maafisa Tarafa wa wilaya hiyo, Viongozi wa vyama vya siasa pamoja na waandishi wa Habari
Credits: Lindi Yetu Blog
Post a Comment