Akiongea kwa
uchungu , Spika wa Bunge bi Anne Makinda amewashambulia wabunge leo asubuhi na
kuwaambia suti zao walizovaa haziendani na matusi yanatoka katika vinywa
vyao ambayo yeye ameshindwa kuyataja kutokana kwa madai kuwa mdomo wake
hauwezi kutamka matusi hayo.....
Makinda
amesema matusi ndiyo yamekuwa yakitawala katika midomo ya wawakilishi hao na
kuacha hoja inayojadiliwa hewani....
Spika wa bunge amekwenda
mbali zaidi na kuwaambia wabunge hao kwamba hataangalia chama endapo mbunge
atavunja kanuni za bunge kwa kuwa kanuni za bunge zinampa nafasi ya kuita polisi
na kuja kumchukua mbunge huyo kwa hatua za kisheria.
Makinda amesema ametumiwa
sms ambayo mtumaji amedai hatokaa tena na familia yake kuangalia bunge labda
ajifungie chumbani.



Post a Comment