Mkuu wa Jeshi
la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja, akikata utepe kuzindua rasmi
jukumu la kuwasafirisha Mahabusu kutoka Gerezani kwenda Mahakamani na kurudi
Gerezani kwa Mkoa wa Arusha. Katikati ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya
Arusha, Aisha Nyerere akipongeza uzinduzi huo. Uzinduzi huo ulifanyika katika
Gereza Kuu Arusha.
Mkuu wa Jeshi
la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja (kushoto) akisalimiana na Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, Aisha Nyerere baada ya kutoa hotuba ya
uzinduzi wa mabasi manne na gari ndogo moja (pick-up) kwa ajili ya
kuwasafirishia mahabusu toka gerezani kwenda mahakamani na kurudi gerezani kwa
mkoa wa Arusha. Uzinduzi huo ulifanyika katika Gereza Kuu
Arusha.
Mkuu wa Jeshi
la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja akitoa hotuba yake kabla ya
kuzindua mabasi manne na gari ndogo moja (pick-up) kwa ajili ya kuwasafirishia
mahabusu toka gerezani kwenda mahakamani na kurudi gerezani kwa Mkoa wa Arusha.
Katika hotuba yake mkuu wa jeshi hilo aliwataka maofisa magereza wa mkoa huo
wawe makini kuyatunza magari hayo. Uzinduzi huo ulifanyika katika Gereza Kuu
Arusha.
Sehemu ya magari matano ya
kuwasafirisha Mahabusu yaliyozinduliwa na Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini,
Kamishna Jenerali John Minja, katika hafla iliyofanyika Gereza Kuu la
Arusha
Post a Comment