Featured
    KWA HABARI NA MATANGAZO EMAIL : pbuyegu2@gmail.com ... Get a superior results by advertising with us by E- Mail us pbuyegu2@gmail.com We will bring Your Business to Light

    Featured Posts

Loading...

MNYAMA MBELE YA WANAJESHI WA RUVU SHOOTING TAIFA, SAA KUMI JIONI LAIVU BILA CHENGA!!

 
IMG_7706
JULIO KUSHOTO AKIWA NA MSEMAJI WA SIMBA EZEKIEL KAMWAGA
***********
Wekundu wa Msimbazi Simba leo wana kibarua kizito uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam pale watakapokuwa wanaoneshana kazi na vijana wa Charles Boniface Mkwasa “Master” klabu ya Ruvu Shooting katika mchezo wa ligi kuu soka Tanzania bara.
Mchezo huo unatarajiwa kuwa wa vuta ni kuvute kutokana na ukweli kwamba Simba kwa sasa wanahitaji kulinda heshima yao baada ya kupoteza taji lao msimu huu na kuwapa mahasimu wao wa jadi, Dar Young Africans, wakati nao Shooting wanahitaji kupata pointi tatu muhimu ili kujiweka nafasi nzuri zaidi katika msimamo.
Akizungumza na mtandao huu, Kocha msaidizi wa Simba Jamhuri Kiwhelo “Julio” alisema kikosi cha Simba kipo salalama na leo kama ilivyo kawaida kwao vijana wengi wataanza kikosi cha kwanza kupepetana na wanajeshi hao.

“Simba iko safi na sasa tunajenga wachezaji, kocha anatarajia kuwapanga vijana wadogo kama kawaida na tunaamini watacheza soka maridhaWa kama walivyofanya mechi za nyuma”. Alisema Julio.
Julio aliwataja baadhi ya nyota wao makinda wanaotaraji kucheza katika mechi ya leo ya kukata na shoka maeneo ya Chang`ombe uwanja wa taifa.
“Unajua kwa sasa huwezi kuitaja simba bila kuwataja akina Kapombe, Seseme, Singano, Chanongo na wengine wengi, lakini pia tutatumia baadhi ya mafaza kuiwakilisha Simba ambayo kwa sasa tumepoteza ubingwa ila tunahitaji heshima”.
Julio aliwataka mashabiki wa Simba kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu yao kwani kikosi kipo na morali kubwa.
Kwa uande wa Shooting walisema wamekamilisha taratibu zote za kumfunga mnyama.
Akizungumza kwa kujiamini Afisa habari wa klabu huyu Masau Bwire alisema licha ya Simba kutangaza kulinda heshima katika mechi zilizosalia, lakini wao wanajua kuwa lazima wawafunge katika mechi ya leo.
“Sisi tuko sawa usipime, kocha Mkwasa na Suleiman Msungwe wamewaandaa vijana kwa kushindana, leo lazima mnyama afanyiwe kitu mbaya taifa, Shooting ni timu nzuri na wao wanajua sana shughuli yetu, tunataka watanzania walijue hilo”. Alisema Masau.
(Na Baraka Mpenja wa Fullshangwe Dar es salaam)
Download Our App

Post a Comment

CodeNirvana

BLOG RAFIKI

© Copyright EMMANUEL SHILATU - BREAKING NEWS BLOG
Back To Top